Featured • Kimataifa

MIJADALA YA CATA KUWA CHACHU YA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA ZA KODI TANZANIA – CG MWENDA

Written by Alex Sonna

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema mijadala ya Mkutano wa 46 wa CATA itakuwa chachu ya kuboresha zaidi huduma za kodi nchini. Ameyasema hayo akiongoza ujumbe wa CATA ulipotembelea Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya programu ya mkutano huo ulioanza tarehe 5–9 Oktoba 2026.

Bw. Mwenda amesema ziara hiyo imewapa Makamishna fursa ya kujifunza uzoefu wa EAC katika matumizi ya teknolojia, ubadilishanaji wa taarifa na uboreshaji wa mifumo ya Forodha, maeneo yanayochangia kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kurahisisha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema TRA itaendelea kutumia maarifa na uzoefu unaopatikana kupitia mijadala ya CATA katika kuboresha huduma kwa walipakodi, kurahisisha ulipaji wa kodi na kuimarisha ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo ya Taifa.

About the author

Alex Sonna