Jumanne, Novemba 24, 2026
HABARI MPYA
Kitaifa

NDEJEMBI AKAGUA UJENZI WA SOKO LA KIRUMBA, MRADI WAFIKIA ASILIMIA 76.6

 

 

Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo amekagua ujenzi wa Soko la Kirumba, Wilayani Ilemela, Jijini Mwanza, unaotekelezwa chini ya Mradi wa Uendelezaji wa Miji Tanzania (TACTIC). Mradi huo wa Shilingi bilioni 14.7, unaojumuisha barabara ya kilomita 2.9 inayoelekea sokoni, umefikia asilimia 76.6 na unatarajiwa kukamilika Januari 2027.

Makamu wa Rais ameonesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo, na kupongeza kwa usimamizi mzuri, ambapo amehimiza kuendelea kumsimamia mkandarasi kwa ufanisi bila kumbembeleza ili aweze kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Wakati huohuo; Mhe. Ndejembi amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CP Salum Hamduni kufuatilia na kuhakikisha Mkandarasi anawasilisha makato yote ya NSSF wanayokatwa Wafanyakazi kila mwezi kwa mujibu wa Sheria, baada ya wafanyakazi kulalamika kukatwa fedha zao na makato yao kutofikishwa kwenye Mfuko wa NSSF kwa wakati.