Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mb. amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Czech, Mhe. Tomio Okamura, tarehe 23 Novemba, 2026.
Katika Kikao hicho, pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu kuimarisha ushirikiano wa Kibunge na kiuchumi hususan katika uwekezaji nchini Tanzania ili kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Hii ni pamoja na ushirikiano na sekta binafsi katika ujenzi wa reli ya metro katika miji mikubwa.
Mhe. Spika ametumia fursa hiyo pia kumwalika Spika Okamura kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania akiambatana na Waziri wa Uchukuzi wa nchi hiyo.
Katika ziara hiyo Mhe. Spika ameambatana na Katibu wa Bunge Ndg. Baraka Leonard na Wabunge wengine sita akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso, Mb.


