Uncategorized

WAZIRI NDALICHAKO ATAKA WELEDI NA NIDHAMU KWA WATUMISHI 

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo na makadirio ya bajeti mwaka 2022/2023 kilichofanyika leo Machi 22,2022Jijini Dodoma,

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  Prof. Jamal Katundu ,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo na makadirio ya bajeti mwaka 2022/2023 kilichofanyika leo Machi 22,2022Jijini Dodoma,

Mwenyekiti wa Baraza la TUGHE tawi la Ofisi hiyo Bw. Godfrey Chacha,akielezea majukumu ya baraza lake wakati wa  ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika  leo Machi 22,2022Jijini Dodoma.

Watumishi na wafanyakazi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo na makadirio ya bajeti mwaka 2022/2023 kilichofanyika leo Machi 22,2022Jijini Dodoma,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Barza la Wafanyakazi katika ofisi hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi. Kulia ni Katibu Mkuu kutoka katika ofisi hiyo Prof. Jamal Katundu kilichofanyika leo Machi 22,2022Jijini Dodoma,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo na makadirio ya bajeti mwaka 2022/2023 kilichofanyika leo Machi 22,2022Jijini Dodoma,

……………………………………

Na Alex Sonna – DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amewataka Viongozi na Watumishi katika ofisi hiyo kuzingatia weledi, nidhamu na maadili ya utumishi wa umma ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Hayo ameyasema leo Machi 22, 2022 jijini Dodoma wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo na kupokea pamoja na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo na makadirio ya bajeti mwaka 2022/2023

Prof.Ndalichako amewahimiza viongozi na watumishi kufanya kazi kwa kufuata misingi na maadili ya utumishi wa umma katika kuhudumia wananchi kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Ameeleza kuwa, wajibu wa kila mtumishi kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu huku akisisitiza uwepo wa mabaraza ya wafanyakazi katika maeneo ya kazi ambayo yamekuwa ni chachu ya kuongeza ufanisi na tija kwa wafanyakazi kwa kuimarisha ushirikiano.

“Serikali imeonyesha juhudi kubwa za kuhakikisha watumishi wote wa Umma wanafanya kazi kwa weledi na nidhamu kwa lengo la kufikisha huduma bora kwa wananchi wote,” amesema 

“Ni matumaini yangu kwamba kupitia mabaraza haya ya wafanyakazi tutaweza kuimarisha mshikamano, kufanya kazi kwa umoja, hivyo tuhakikishe ushauri na mawazo yatakayotolewa na watumishi katika mabaraza itakuwa ni chachu ya kuhamasisha tija katika utekelezaji wa majukumu yetu sambamba na kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo, amesema Prof. Ndalichako

Ameongeza kuwa, Ofisi  hiyo imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha mwaka moja wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo shughuli mbalimbali katika sekta hiyo zimefanyiwa kazi kwa wakati.

“Tuendelee kuhakikisha maelekezo yote yanayotolewa na Mheshimiwa Rais katika kukuza uchumi wa Taifa letu ili uwafikie wananchi kikamilifu yanafanyiwa kazi kwa ufanisi na wakati,” amefafanua Prof. Ndalichako

Hata hivyo Prof.Ndalichako amewataka viongozi wa TUGHE kuendelea kushirikiana na Uongozi wa ofisi hiyo pamoja na watumishi. Pia aliwasihi watumishi kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Aidha amewahamasisha watumishi kuwa wabunifu na kushirikiana kwa pamoja ili kuendelea kuimarisha utendaji kazi wa majukumu yao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la TUGHE tawi la Ofisi hiyo Bw. Godfrey Chacha alieleza kuwa Baraza pamoja na majukumu mengine lina kazi ya kupanga mipango na kushauri viongozi na watumishi kuhusu ufanisi wa kazi na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kuhakikisha kuwa huduma zinatolewa kwa wakati na kwa ubora unaokubalika ili kufanya kazi kwa uadilifu.

About the author

mzalendoeditor