Uncategorized

MWAKIBETE ATAKA MICHANGO YA WATUMISHI WA SEKTA YA UCHUKIZI  IWASILISHWE KWA WAKATI 

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Uchukuzi (hawapo pichani), wakati akifungua baraza hilo lililofanyika leo Machi 22,2022 Jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta ya Uchukuzi (hawapo pichani), wakati akifungua baraza hilo lililofanyika leo Machi 22,2022 Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Uchukuzi), Bw Gabriel Migire,akifafanua jambo kwa wajumbe wa baraza la Wafanyakazi Sekta ya uchukuzi (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo lilifanyika  leo Machi 22,2022  Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara hiyo anayesimamia Sekta ya Uchukuzi, Atupele Mwakibete (hayupo pichani) wakati wa akifungua baraza hilo lililofanyika leo Machi 22,2022 Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete (wa tatu waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Sekta hiyo mara baada ya kuzindua baraza hilo leo Machi 22,2022,Jijini Dodoma.

………………………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

NAIBU  Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Atupele Mwakibete,amewataka viongozi wa wizara hiyo kuwasilisha michango ya watumishi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati ili kuwaondolea adha wastaafu ya kukosa mafao yao kwa wakati.

Hayo ameyasema leo Machi 22,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa baraza la Wafanyakazi lililowakutanisha kwa ajili ya kujadili masuala ya wafanyakazi na kupitia mpango wa Bajeti kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.

Mwakibete amesema kuwa kitendo cha michango ya watumishi wa umma kutowasirishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kumekuwa kunasababisha malalamiko mengi kwa wastaafu kukosa mafao kwa wakati.

“Kwa kipindi kifupi ambacho nimeingia katika wizara hii nimekutana na malalamiko mengi juu ya wastaafu kukosa mafao yao na kusababisha kuwa na maisha magumu.

“Hakikisheni mnashughulikia malalamiko ya watumishi sehemu mnazozisimamia ili kuweka usawa na utendaji kazi mzuri kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kupewa nafasi za kujiendeleza kielimu”, amesema Mwakibete.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Gabriel Migire, amesema kuwa  lengo la kikao hicho ni kujadiri utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 pamoja na bajeti ya 2022/2023.

“Baraza hili linakutana hapa kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa mpango na Bajeti ya Sekta ya Uchukuzi kwa mwaka 2020/2021 ikiwa ni pamoja na masuala mbalimbali yanayowahusu watumishi ”,amesema Bw.Migire

About the author

mzalendoeditor