Jumatatu, Novemba 23, 2026
HABARI MPYA
Michezo

HISPANIA YAFANYA MAUAJI WC U_17

Timu ya taifa ya Hispania chini ya umri wa miaka 17 (La Rojita) imeonyesha ubabe katika fainali za Kombe la Dunia la FIFA U-17 zinazoendelea nchini Qatar baada ya kuichakaza Fiji kwa kipigo kizito cha mabao 15-0 na kujikatia tiketi ya kufuzu hatua ya mtoano. 

Katika mvua hiyo ya mabao, mshambuliaji Rafa Cruz aling’ara zaidi kwa kufunga mabao matano peke yake, huku Roberto Tomás na Guillermo Trujillano kila mmoja akiondoka na mpira wake baada ya kupiga hat-trick (mabao matatu).

Mabao mengine ya Hispania yaliwekwa kimiani na Jorge Domínguez (mawili), Marco Company na Yeremaiah Santos, ushindi ambao unaiweka Hispania bao moja tu nyuma ya rekodi ya kihistoria ya ushindi mnono zaidi katika mashindano hayo (16-0 iliyowekwa na Morocco dhidi ya New Caledonia). 

Vijana hao wa Hispania sasa wanakwenda hatua ya mtoano wakiwa na morali ya juu na ujumbe mzito kwa wapinzani wao kuwa wamekuja Qatar kuchukua ubingwa!

Mbali na ushindi mnono wa Hispania 15-0 Fiji, matokeo ya mechi nyingine za Kombe la Dunia la FIFA U-17 zilizochezwa leo Jumatatu, Novemba 23, 2026:

Tajikistan 0 – 4 Croatia (Kundi F)

Uzbekistan 6 – 2 Jamaica (Kundi E)

Senegal 9 – 0 Cuba (Kundi F)