Jumatatu, Novemba 23, 2026
HABARI MPYA
Featured

KITUO CHA MTAMBO WA NYUKLIA CHASHAMBULIWA NA URUSI

Kituo cha Mtambo mkubwa wa Nishati ya Nyuklia Barani Ulaya kilichoko Ukraine   kimelengwa katika mashambulizi ya Urusi usiku wa kuamkia leo Ijumaa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba ametaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo hilo ili kuepusha Maafa

Msemaji wa Mtambo huo wa Zaporizhia  , Andrei Tuz amesema shambulio la makombora lililofanywa na Vikosi vya Urusi, limesababisha Moto kuwaka katika mojawapo ya sehemu ya kituo hicho