Featured Kitaifa

MANGULA AONGOZA MAZIKO MWENYEKITI WA CCM KONDOA

Written by mzalendoeditor

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Philip Mangula,akizungumza wakati akiwaongoza mamia ya wakazi wa wilaya Kondoa kwenye maziko ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Mohamed Kova.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Antony Mtaka,akizungumza wakati wa maziko ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kondoa  Mohamed Kova.

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk.hamis Mkanachi ,akizungumza wakati wa maziko ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kondoa  Mohamed Kova.

Aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, akizungumza pamoja na kuwashukuru viongozi na wananchi waliojitokeza kwenye mazishi ya aliyekuwa kaka yake Mzee Mohamed Kova

Mtoto Wa Marehemu Mzee Mohamed Kova, Ibrahim Kova akisoma wosia wa baba yake katika mazishi yaliyofanyika Kondoa nyumbani kwa marehemu.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Mhe. Philiph Japhet Mangula (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka (kushoto) wakiwa kwenye mazishi ya Mzee Mohamed Kova ambaye alizikwa jana 4 Machi 2022. Kondoa

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye msiba wa Mzee Mohamed Kova ambaye alizikwa jana 4 Machi 2022. Kondoa

…………………………………………………..

Na Bolgas Odilo-KONDOA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Philip Mangula juzi  ameongoza mamia ya wakazi wa wilaya Kondoa kwenye maziko ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Mohamed Kova.

Akizungumza wakati akitoa salamu za chama Mangula alisema CCM imempoteza kiongozi bora ambaye pengo lake halitazibika.

“Mungu wa ajabu sana zimepita siku 30 tu tangu nilipokutana na Kova enzi za uhai wake na alinitania kwasababu nilikuwa mwalimu wake wa chuo Cha uongozi Kivukoni wakati alipoteuliwa kushika wadhifa wa Katibu tarafa”alisema

Aidha Mangula alisema Kova enzi za uhai wake alikuwa kiongozi na mwanasiasa mkomavu na sasa amemaliza safari yake ya duniani naameondoka na heshima yake.

Kadhalika, aliwataka wanachama wa cha hicho wilya ya Kondoa kuenzi kwa kuendeleza mema aliyokuwa akifanya wakati wa uhai wake.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka, akitoa salamu za mkoa alisema Mzee Kova atakumbukwa kwa mambo mengi hasa katika Chama na serikali.

“Kova amelala tunahubiri ujenzi wa misikiti, madarasa na vitu vingi naomba msiba huu uwe funzo kwetu tuhakikishe tunafanya mambo mazuri ili siku unapokufa unawapunguzi viongozi wa dini kutunga uongo katika mahubiri ya msiba wako”alisema Mtaka

Mtaka alisema seriklai pamoja na chama kimepoteza mtu ambaye matendo yake yataishi milele.

“Tuendeleee kumtunzia heshima na kuhakikisha nyumba yake inatunzwa”alisema Mtaka

Pia, Mtaka alisema kutoka na urafiki aliokuwa nao na marehemu atahakikisha siku yake ya arobaini yake analeta Ng’ombe.

“Nakama ratiba zangu zitakuwa hazijanibana nitakuja kwasababu kiongozi ambaye aliofanya kazi nzuri na tunawatoa pole Kwa serikali,CCM, na familia na tunaomba mpate kiongozi mwingine ambaye ataziba pengo lake”alisisitiza Mtaka

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk.Hamis Mkanachi alisema msiba huo ni mkubwa na ni pigo kubwa kwasababu wamepoteza kiongozi mahili na mzalendo.

Alisema marehemu Kova alikuwa kiongozi ambaye alizifanya kazi zake kwa weledi hivyo maono yake na farsafa zake zitaendelea kuishi milele na wanamuombea kwa mwenyezi mungu ampumzishe kwa amani.

“Msiba huu ni mkubwa na Kondoa tumepata pigo kwasababu tumepoteza kiongozi mahili ambaye aliipenda nchi yake na kufanya kazi kwa uzalendo na tunamuombea kwa mwenyezi mungu ampe pumziko la milele amina”alisema

Akisoma wasifu wa marehemu mtoto wake Ibrahim Kova, alisema baba yake alizaliwa Desemba 28 mwaka 1942 katika kijiji Cha Chakwe Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.

Alisema baba yake amepita katika ngazi mbalimbali za uongozi na hadi umauti ulipomkuta alikuwa ni mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kondoa.

“Mzee Kova wakati wa uhai wake amelitumikia Taifa katika nyazifa mbalimbali za uongozi ikiwemo Chama na serikali na alikuwa mzalendo tunamuombea kwa Mungu apumzike kwa amani “alisema

Akitoa salamu kwa niaba ya familia mdogo wa marehemu Suleiman Kova, alisema anashukuru kwa viongozi wa Chama na serikali kuwakimbilia katika wakati huu mgumu.

“Nashukuru Makamu mwenyekiti Mzee Mangula kwa kuja kuungana nasi katika kipindi hichi kigumu nakumbuka juzi usiku saa nane kaka alinipiga akasema anaumwa sana na kwa hali ilivyo anaona kuwa hata pona hivyo amepiga kuniaga na kunikabidhi kuilea familia ya Mzee Kova kwa sababu mie ndiye nilikua makamu mwenyekiti wa familia”alisema Kona

About the author

mzalendoeditor