MKURUGENZI wa Maendeleo ya Uwekezaji na Biashara wa shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bw.William Ngenya, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa sera yake ya ubia unaotarajiwa kufanyika Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.Kushoto ni Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika hilo, Muungano Saguya.
………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), linatarajiwa kuzindua sera ya ubia mnamo Novemba 14 mwaka 2022 unaolenga masuala mbalimbali ya uwekezaji ambapo kwa miaka mitano inategemewa kuwa na miradi 200 ya ubia yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 400.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 20,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uwekezaji na Biashara wa Shirika hilo, Bw.William Ngenya, amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Bw.Ngenya amesema kuwa sera hiyo ilianza kufanya kazi tangu mwaka 1993 na hapo katikati iliweza kufanyiwa maboresho mara nne na hayo yote yamekuwa yakilenga kuweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji lakini pia kuipa shirika hisa zaidi katika miradi.
“Tunaungana na Rais Samia Suluhu Hassan kuleta wawekezaji wa ndani na nje ili uchumi ukue zaidi, tumeboresha sera kwa kuweka vitu vinne ambapo Mwekezaji ataangalia,”amesema Ngenya.
Amesema kuwa tangu kuanza kwa utaratibu huo jumla ya miradi 111 ilitekelezwa ikiwa na thamani ya bil.300,ambapo katika miradi hiyo miradi 81 yenye thamani ya sh.bilioni 240 imekamilika na kuanza kutumika huku miradi 30 yenye thamani ya bil.60 inaendelea kukamilishwa.
Miradi hii imechangia upatikanaji wa ajira, kuboresha mandhari ya miji yetu,kuongeza mapato ya shirika,kuongeza wigo wa kodi za serikali, kuongeza maeneo kwaajili ya biashara na makazi na kuipanga miji yetu”alisema.
“Sasa thamani ile ya bililioni.300 ile thamani ya hisa za shirika kwenye miradi ambapo hisa hizo katika miradi hiyo kuna za asilimia 25 kwenye baadhi ya miradi mpaka asilimia 50, hivyo dhamani ya miradi yote kwa ujumla zikiwemo hiza za wabia ni zaidi ya Trilioni. 1.2”almesema.
Aidha amesema kuwa shirika kuweka ardhi na fedha kama mtaji na mbia anaweka fedha halafu tunatekeleza mradi kwa pamoja ,nahii ni kwa ile miradi mikubwa ambayo thamani yake inazidi bil.50 na zaidi.
Ametaja ,Kujenga,kuuza na kugawana ambapo shirika linaweka ardhi na mbia anaweka fedha ambapo jengo linajengwa halafu linauzwa lote na shirika na mbia wanagawana mapato yaliyotokana nakuuza jengo hilo kutokana na umiliki wa hisa kwenye mradi.
“Nne ,Shirika linatoa ardhi kwa mkataba wa miaka 10 hadi 30 ,halafu mbia anajenga na kuendesha jengo lile na baada ya muda wa mkataba kuisha anarudisha jengo lile kwa NHC”amesema.
Hata hivyo ameeleza kuwa Katika utekelezaji wa sera hiyo, Shirika hilo litalazimika kuvunja majengo yake ya zamani yaliyopo katika maeneo ya katikati ya Miji ili kufanyika uwekezaji wa majengo makubwa.
Kwa upande wake Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Muungano Saguya amesema kuwa uzinduzi wa sera ya ubia unaenda kufungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya nyumba na kwa hakika wanaunga mkono maono na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvutia uwekezaji nchini kwa kuruhusu sekta binafsi ambayo ni injini ya kuleta maendeleo ili iwekeze mitaji yao kujenga uchumi wa taifa .
”Kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kampuni binafsi za ndani na nje ya nchi kushiriki katika uzinduzi huo ikiwamo Diaspora na wawekezaji wa kimataifa.”amesema Bw.Saguya
Bw.Saguya amesema kuwa wanatarajia kuwa na washiriki 1000 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ,vyama na bodi za kitaaluma pamoja na wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi.
MKURUGENZI wa Maendeleo ya Uwekezaji na Biashara wa shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bw.William Ngenya, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa sera yake ya ubia unaotarajiwa kufanyika Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.Kushoto ni Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika hilo, Muungano Saguya.
MKURUGENZI wa Maendeleo ya Uwekezaji na Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bw.William Ngenya, akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu uzinduzi wa sera yake ya ubia unaotarajiwa kufanyika Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.Kushoto ni Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika hilo, Muungano Saguya.
MENEJA Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya,akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa sera ya ubia unaotarajiwa kufanyika Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.Kushoto ni MKURUGENZI wa Maendeleo ya Uwekezaji na Biashara wa Shirika hilo,Bw.William Ngenya.