Featured Kitaifa

UTEUZI:RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu  Hassan amemteua Prof. Said Shehe Aboud kuwa Mkurugenzi Mkuu wa  Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). 

Prof. Aboud ni Profesa Mshiriki na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango,  Fedha na Utawala, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam. 

Prof. Aboud anachukua nafasi ya Prof. Yunus Daud Mgaya ambaye  amemaliza muda wake mwezi Septemba, 2022. 

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Oktoba, 2022. 

Zuhura Yunus 

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

About the author

mzalendoeditor