Na.OWM- TAMISEMI, Iringa
Mikoa ya Manyara na Arusha imeanza vizuri Mashindano ya UMITASHUMTA baada ya timu zao kupata ushindi katika michezo iliyochezwa leo tarehe 11 Juni 2026.
Kwa upande wa Wasichana, timu ya Mkoa wa Manyara imeifunga Morogoro kwa Seti 3-0 katika mchezo uliochezwa viwanja vya chuo cha ualimu Kleruu Manispaa ya Iringa.
Michezo mingine ilimalizika ka Katavi kushinda Seti 3-1 dhidi ya Rukwa, Dodoma ikaishinda Kageri 3-0 na Wenyeji Iringa wakapoteza 3-0 kwa Singida.
Kwa upande wa Wavulana Singida imeifunga Mtwara seti 3-0, Pwani ikashinda 3-2 dhidi ya Kigoma, na baadae Geita ikaishinda Morogoro 3-0 na Arusha wakaishinda Songwe 3-2.
Mchezo wa wavu mwaka huu yanahusisha jumla ya team 51, kati yake 24 zikiwa ni za wasichana na 27 wavulana.
