Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto CGH, amewasili nchini Tanzania kwa Ziara ya Kitaifa ya Siku Mbili Mei 4 na 5, 2026.
Mheshimiwa Ruto atapokelewa kwa gwaride la heshima na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam ambapo pia watafanya mazungumzo ya uwili ili kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya.
Mapema kesho, Mei 5, 2026 Mheshimiwa. Ruto atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma kabla ya kuhitimisha ziara yake.
Mhe. Ruto amepokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dr. Bernard Kibesse, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Catherine Karemu pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
