
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 6, 2026 amemtembelea na kumjulia hali mchezaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa akiwa uwanjani.
Pacome alipata majeraha hayo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga SC na JKT Tanzania, uliochezwa hivi karibuni katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Mashabiki wa Yanga SC pamoja na wapenzi wa soka kwa ujumla wameendelea kumtakia Pacome nafuu ya haraka ili aweze kurejea uwanjani baada ya kukamilisha matibabu.