Kitaifa

BMH YAENDELEA KUPANDIKIZA BETRI KWENYE MOYO

Written by mzalendo

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma imefanya upandikiza betri kwenye moyo kwa watu watatu.

Upandikizaji wa betri kwenye moyo ambao kitaalamu unaitwa _pacemakers_ _implantation_ unafanyika kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa kwa mtu wa kawaida ambayo ni 60-100 kwa dakika.Wengi wao huwa ni chini ya 40.

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa BMH, Daktari Bingwa wa Moyo, Happiness Kusima, amesema leo kuwa BMH imefikisha upandikizaji kwa watu 18 toka huduma ianzishwe mwaka 2021.

“Jana tumepandikiza watu watatu (3), leo tumepandikiza watu wawili,” amesema Daktari huyo Bingwa wa Moyo.

Dkt Happiness amesema upandikizaji huu umefanyika kwenye kambi ya Madaktari Bingwa wa Moyo wa BMH kwa kujengewa uwezo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya jijini Dar es Salaam.

About the author

mzalendo