Kitaifa

WANASHERIA MNA WAJIBU WA KUITETEA SERIKALI’ MCHENGERWA

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema wanasheria wote walioko katika sekta ya sheria kujua wanawajibu wa kuitetea na kulinda Serikali dhidi ya maadui wanaweza kuhihuma Serikali.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kilichofanyika tarehe 18.12.2023 kwenye Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dodoma.

Pia amewataka kuwa wazalendo, waadilifu, kufanya kazi kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoe kwani Serikali ikianguka wote tutakuwa tumeanguka.

Mchengerwa pia ameiomba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa karibu na wanasheria wa mamlaka za serikali za mitaa ili kusaidia uboreshaji wa sheria ndogo na kanuni zinatotumika kwenye halmashauri.

Alisema kwa sasa kumekuwa na malalamiko ya kuwapo sheria ndogo na kanuni ambazo hazizingatii katiba na sheria mama hiyo kuwatesa wananchi hususani wa vijijini.

Awali, Mwenyekiti wa Baraza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi alisema Ofisi yake ina upungufu wa watumishi 285 huku asilimia 85 ya Watumishi waliopo wamepatiwa vifaa vya TEHAMA hivyo kupunguza mlundikano wa shughuli mezani na kurahisisha uendeshaji wa mashauri kwa njia ya mtandao.

Alisema pia wanasheria 3,359 wamesajiliwa kwenye mfumo wa Chama Cha Mawakili wa Serikali na kati ya hao wanasheria 307 ambao ni asilimia 9 wako kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

About the author

mzalendo