Kimataifa Kitaifa

WANANCHI KARAGWE WAPEWA ELIMU UMUHIMU WA LISHE NA CHANJO YA  SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI(HPV) .

Written by mzalendoeditor

Na.Elimu ya Afya kwa Umma.

Jumla ya washiriki 107 wameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe   Wilaya  ya Karagwe Mkoani Kagera ambapo 
katika maadhimisho hayo mwitikio wa wanaume umekuwa mkubwa .

image.png
image.png
image.png
Pichani ni Matukio mbalimbali katika  Maadhimisho ya siku ya Afya na Lishe Wilaya ya Karagwe ,jumla ya washiriki 107 wameshiriki, .

Hata hivyo, Wilaya ya Meatu  Meatu Mkoani Simiyu nayo haikuachwa nyuma katika maadhimisho hayo ambapo Afisa lishe  katika wilaya hiyo  Anna Msangi kwa kushirikiana na watoa huduma wametumia fursa ya maadhimisho hayo kutoa elimu ya afya kuhusu lishe, umuhimu wa chanjo ya HPV kwa watoto na kuhamasisha chanjo kwa watoto walioacha mtiririko wa chanjo huku wanafunzi  10 Shule ya Msingi  Isingiro    Wilaya    Kyerwa  Mkoa  Kagera   nao pia  wakipata  chanjo  ya Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV) 

image.png
image.png

image.png
Afisa Lishe Wilaya ya Meatu pamoja na watoa huduma wakitoa elimu ya Afya  kuhusu lishe, umuhimu wa chanjo ya  Saratani ya Mlango wa Kizazi(HPV )kwa watoto na kuhamasisha chanjo kwa watoto walioasi chanjo leo Tarehe 13/3/23 katika hospital ya Wilaya ya Meatu
 
image.png
Wanafunzi  10  wa Shule ya msingi  Isingiro Wilaya    Kyerwa  Mkoa  Kagera waliopata  chanjo  ya Saratani ya Mlango wa Kizazi  (HPV)    
Ikumbukwe kuwa siku ya Maadhimisho ya Afya na Lishe huadhimishwa kwa lengo la kuikumbusha jamii umuhimu wa kuzingatia kanuni bora za Afya ikiwemo kuzingatia lishe bora ili kuepukana na udumavu, unene uliopitiliza, na umuhimu wa kufanya mazoezi.

About the author

mzalendoeditor