Featured Kitaifa

MERU DC na EMAC WASHIRIKIANA KUTOA ELIMU, MBEGU NA MITI YA MATUNDA KWA WANAFUNZI .

Written by mzalendoeditor

Na.Elimu ya Afya kwa Umma

Katika kuendelea kuadhimisha siku ya Afya na Lishe, Wataalamu wa uelimishaji kutoka katika Halmashauri ya Meru DC kwa kushiriana na Shirika lisilo la kiserikali la EMAC wametoa elimu pamoja na Miche ya Miti ya Matunda na Mbegu za mboga za majani kwa Wanafunzi wa Klabu za utunzaji wa mazingira na Usafi kutoka katika shule za Msingi na Sekondari kwenye Kata za Ikiliding’a na Oltrument katika Halmashauri ya Meru DC , Mkoani Arusha

Ugawaji huo wa miti ya matunda na mbegu za mboga za majani umefanyika kwa lengo la kuwajengea uelewa Wanafunzi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kula mboga za matunda kwa wingi kwa ajili ya kujenga Afya zao na kujikinga na Magonjwa mbalimbali, Jumla ya wanachama 45 wa Klabu hizo wamepatiwa miche na mbegu hizo wakiwemo walimu wa Afya kutoka katika shule hizo

Pamoja na zoezi hilo kufanyika pia Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mrina katika Kata ya Oltrument waliandaa igizo lililokuwa limebeba ujumbe kuhusu madhara yatokanayo na uchafu wa mazingira ambapo Jumla ya Wanafunzi 869 walipatiwa Elimu hiyo.

About the author

mzalendoeditor