Featured Michezo

MAN UNITED YAICHAKAZA MAN CITY LIGI KUU YA ENGLAND

Written by mzalendoeditor

MANCHESTER Manchester United wametoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao Manchester City katika mchezo was Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Man City walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa  Jack Grealish dakika ya 60, kabla ya Bruno Fernandes kusawazisha dakika ya 78 na Marcus Rashford kufunga la ushindi dakika ya 82.
Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 38 na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja tu Manchester City baada ya wote kucheza mechi 18.
Ni Arsenal ndio wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 44 za mechi 17.

About the author

mzalendoeditor