Featured Kitaifa

TGNP,WABUNGE VINARA WA JINSIA WAJADILI CHANGAMOTO ZA WANAWAKE DODOMA

Written by mzalendoeditor

 Mwezeshaji kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) Deogratius Temba,akitoa mada wakati wa semina kwa wadau pamoja na Wabunge wanawake vinara wa jinsia Bungeni Dodoma yenye lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakutana wanawake mafunzo yaliyoandaliwa na mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) 

Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake Mhe.Magreth Sitta,akizungumza wakati mafunzo wadau pamoja na Wabunge wanawake vinara wa jinsia Bungeni Dodoma yaliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum CCM Mhe.Najma Giga,akichangia mada wakati wa Semina ya wabunge wanawake vinara wa jinsia pamoja na wadau bungeni Dodoma yaliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mhe.Esther Matiko,akichangia mada wakati wa Semina ya wabunge wanawake vinara wa jinsia pamoja na wadau bungeni Dodoma yaliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Mwanaharakati Kishapu DC Kaifa Ituja,aakitoa mawazo yake wakati wa Semina ya wabunge wanawake vinara wa jinsia pamoja na wadau bungeni Dodoma iliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum CCM  Mhe. Fatma Toufiq,akichangia mada wakati wa Semina ya wabunge wanawake vinara wa jinsia pamoja na wadau bungeni Dodoma iliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Mbunge Jimbo la Sikonge Mhe.Joseph Kakunda,akichangia mada wakati wa Semina ya wabunge wanawake vinara wa jinsia pamoja na wadau bungeni Dodoma iliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Mwanarakati KC Makumbusho,Monica Alex,akichangia mada wakati wa Semina ya wabunge wanawake vinara wa jinsia pamoja na wadau bungeni Dodoma iliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Sehemu ya wabunge wanawake vinara wa jinsia pamoja na wadau wakifatilia mada mbalimbali wakati wa semina iliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake Mhe.Magreth Sitta,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupewa mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) ambao uliwakutanisha wadau pamoja na Wabunge wanawake vinara wa jinsia Bungeni Dodoma.

Mwezeshaji kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) Deogratius Temba,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwapa mafunzo  wadau pamoja na Wabunge wanawake vinara wa jinsia Bungeni Dodoma ili kujadili changamoto zilizopo.

MWENYEKITI wa Kituo cha Mnalo Lihumbo Kishapu,Rachel Lises,akielezea changamoto wanazokutana nazo wanawake katika maeneo ya vijijini.

Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wanawake Mhe.Magreth Sitta,akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wanawake vinara wa jinsia,wadau wa TGNP mara baada ya kupewa mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP,) yenye lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wanawake Bungeni Dodoma.

…………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

MTANDAO wa jinsia Tanzania (TGNP,) umekutana na wadau pamoja na Wabunge wanawake vinara wa jinsia Bungeni Dodoma na kuwapa mafunzo ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia itakayowanufaisha wanawake na makundi yaliyoko pembezoni ili kuondoa mzigo unaowasumbua wanawake katika masuala ya afya,elimu,maji,haki ya uchumi ,kilimo na ukatili wa kijinsia.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo  Mwezeshaji kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) Deogratius Temba, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yanaibua majadiliano chanya pamoja na kuzipatia ufumbuzi changamoto za masuala mbalimbali ya kijinsia hasa kwa kundi la wanawake, watoto na kundi la wenye ulemavu.

Temba amesema TGNP imeendelea kushirikiana na makundi mbalimbali katika kujadili bajeti kila mwaka kwa mlengo wa kijinsia na kwamba lengo ni kuwa na maendeleo endelevu yenye kujumuisha ustawi wa makundi yote na kudumisha haki za msingi za binadamu.

“TNGP tunafanya kila jitihada zenye lengo la kuboresha sekta za huduma kwa jamii, sekta ambazo kwa kiwango kikubwa zinawagusa wanawake moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ya huduma za afya na elimu hii yote ni kuamsha ari kwa Serikali kutenga bajeti yenye kulenga na kuhamasisha utoaji wa bima za afya kwa gharama sawa na bure kwa wajane wenye uhitaji, wazee na wanawake na kaya masikini nchini,”ameeleza

Temba ameishauri Serikali kuongeza kiasi cha ruzuku ya kila mwanafunzi kutoka Sh. 10,000 ya sasa hadi Sh. 25,000.

Amesema kuwa kiasi hicho kitasaidia shule kujiendesha na kuwezesha huduma mbalimbali kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwapatia taulo za kike wanafunzi wa kike.

“Kiasi cha Sh. 10,000 ni kidogo sana kimekuwa kikitumika kwa zaidi ya miaka 20 sasa hivyo ni wakati mwafaka sasa kuongeza hadi Sh. 25,000 ili kukidhi hali ya mabadiliko ya uchumi kwa sasa na kusaidia kutoa huduma kwa wanafunzi za uji pamoja na taulo za kike ili watoto washiriki masomo bila kukosa”alisema Temba

Aidha ameishauri Serikali kuandaa mwogozo wa bajeti ambao utazilazimisha halmshauri zote nchini kuwa na bajeti zenye mlengo wa kinsia ili kutoa taulo za kike kwa wanafunzi pamaoja kuandaa vyumba vya kujihifadhia mabinti wanapokuwa katika hedhi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Wabunge wanawake Magreth Sitta,amesema kuwa mambo yote ambayo yamewasirishwa kwao na wanajamii hao watayachua na kuendelea kuishauri serikali kuyafanyia kazi.

“Ni jambo la kusikitisha kuona wanawake hawapati maji safi na salama,niwaombe wadau wote wa maendeleo kuendeleza sauti hii ya jamii lakini kwa kushirikiana na sisi wabunge ili kwa pamoja tuweze kuondokana na hii hali,tunatamani kuona hata vituo vya kulelea Watoto wenye changamoto na vituo vya wazee vinapewa maji bila gharama yoyote,”amesema Mama Sitta.

Naye mmoja wa wawakilishi wa mafunzo hayo na mdau wa masuala ya kijinsia kutoka Wilaya ya Kishapu,Mkoa wa Shinyanga Neema Maige amesema anatamani kuona majadiliano yaliyofanyika kwenye mafunzo hayo yanazaa matunda kwa kuwa amechoshwa na changamoto ya uhaba wa maji tikaka Wilaya yao.

Amesema ikiwa idara za maji za mikoa zitawezeshwa,hali ya upatikanaji wa maji kwa wajane, wazee, kwa tozo za viwango vya chini kabisa, au
hata bila tozo yoyote itawezekana.

“TGNP imetuwezesha kukutana hapa na wabunge vinara wa Jinsia ,tuna imani watatusaidi kufikisha sauti ya jamii sehemu husika,tunatamani kilio chetu kisikike ili kuondokana na changamoto za barabara mfano wa barabara ya kilomita 35 kutoka njia panda ya Kolandoto mpaka halmashauri ya wilaya ya kishapu ni mbovu inachangia kupanda kwa nauli,bidhaa za vyakula pamoja na usafiri kuwa mgumu,”amesema

“Wakati mwingine tunapishana na magari ya wagonjwa yamepasuka matairi na kusababisha ajali kutokana na ugumu wa barabara sasa vitu vya namna hii lazima Serikali ifike mahali iangalie namna ya kutusaidia ili na sisi wanawake wa pembezoni tufurahie matunda ya maendeleo,”amesisitiza

Naye Venace Mbena ametumia nafasi hiyo kuishauri Serikali kupitia sekta
ya Kilimo kuhakikisha inaweka mpngo wa kufanikisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uchumi shindanishi, huku akitoa mapendekezo kwa sekta ya kilimo kutenga rasilimali za kutosha kuwalenga wanawake na vijana katika ufikiaji wa mikopo ya masharti au riba nafuu.

“Ili kujikwamua kiuchumi nakuondokananna umasikini uliopo lazima kila mtu ashiriki katika mapambano ,kwa nafasi yangu natamani kuona upatikanaji wa teknolojia sahihi za uzalishaji na uhifadhi, na ufikiaji rahisi wa masoko wezeshi, ufikiaji sahihi wa taarifa za tafiti za mbegu bora na mifumo ya kilimo cha umwagiliaji,kujenga masoko mapya kwenye maeneo yenye mvuto mkubwa kwa bidhaa za wajasiriamali wanawake na vijana,”amesema Mbena

About the author

mzalendoeditor