Featured Kitaifa

MWILI WA PADRE WAOKOTWA UKIWA UMEFUNGWA KWENYE BLANKETI MTONI JIJINI MBEYA

Written by mzalendoeditor
Mwili wa padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya wa Shiriki wa Wamisionari wa Afrika (White Father), Michael Samson umeokotwa jijini Mbeya.
Mwili huo umeokota katika mto Meta maeneo ya Sabasaba jijini humo Jumamosi Juni 11, 2022.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio wamedai kuwa mwili huo ulikuwa umefungwa kwenye blanketi.
Taarifa iliyotolewa na Askofu Mkuu wa jimbo hilo na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Gervas Nyaisonga imeeleza Padre Samson alitoweka Ijumaa Juni 10 mwaka huu katika kituo cha Vijana cha Kanisa Katoliki Mbeya saa 12.30 jioni.
“Alitoweka Juni 10, 2022 katika kituo cha Vijana cha Kanisa Katoliki Mbeya majira ya saa 12.30 jioni na mwili wake kupatikana Juni 11, 2022 saa 4:00 asubuhi maeneo ya Sabasaba jijini Mbeya” imesema taarifa hiyo ya Askofu.
CHANZO MWANANCHI.

About the author

mzalendoeditor