Featured Kitaifa

CHONGOLO ASHIRIKI UCHAGUZI WA VIONGOZI SHINA KILIMANI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwa amejumuika na wanachama wa Shina namba 5 kwa ajili ya kuchagua Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Shina, Tawi la Kilimani, Kata ya Kilimani, Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akipiga kura ya kuchagua Uongozi wa CCM Shina namba 5,Tawi la Kilimani, Kata ya Kilimani, Dodoma.(

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa Shina namba 5 akiwemo Katibu wa NEC,Idara ya Oganaizesheni ya CCM Dkt. Moudline Cyrus Castico wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Shina, Tawi la Kilimani, Kata ya Kilimani, Dodoma.(Picha na Adam H. Mzee/ CCM Makao Makuu)

…………………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo ameshiriki kupiga kura katika shina namba tano kata la Kilimani na kuzindua shina la wakereketwa madereva wa bodaboda na bajaji huku akiwataka kulitumia kwa kazi kusudiwa si kufanya porojo.
Aidha, amewaahidi vijana hao kuwa ndani ya wiki mbili atazungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan ili awape bodaboda moja itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo ameitoa leo April 23,2022 jijini Dodoma wakati akizindua  shina hilo mara baada ya kushiriki zoezi la upigaji kura katika shina namba tano, lililopo kata ya Kata ya Kilimani jijini hapa.
Chongolo amewapongeza vijana hao kwa uamuzi wa kuanzisha tawi hilo huku akiwasisitiza kuwa litumike kwa kazi kusudiwa si kwa ajili ya kupiga porojo zisizo na maana.
“Lengo letu muwe na makazi bora nyinyi na familia zetu hivyo nawaahidi nitamuomba Rais Samia awachangie bodaboda na hesabu ya jioni itakayopatikana ni yenu mtagawana,”amesema
Aidha, Chongolo amewaagiza baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dododoma kwenda kuangalia kama vijana hao wanakopesheka ili wawaingize kwenye mikopo ya halmashauri.
 Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amewataka   madereva hao  kutumia shina hilo vizuri ili liweze kuwainua kiuchumi.
 Shekimweri amewataka kuunda kikundi na kukisajili kitakachowawezesha kupata mikopo na kuahidi kuwapa kipaumbele pindi watakapokamilisha shatri hilo.
katika uchaguzi uliofanyika leo katika shina namba tano lililopo Kata ya Kilimani ambao Katibu Mkuu alishiriki na kupiga kura,Juma Saigwa aliibuka kidedea nafasi ya Mwenyekiti kwa kupata kura 45 sawa na asilimia 90 ya kura zilizopigwa.
Aidha, nafasi ya Katibu ilichukuliwa na Maxmillian Mtabekwa na wajumbe watatu ambao ni Liana Danford, Regina Kalindo na John Msalika ambapo uchaguzi ulifanyika kwa demokrasia na haki hadi kuwapata viongozi hao.

About the author

mzalendoeditor