Featured Kitaifa

MZEE WA MIAKA 95 AUAWA AKITUHUMIWA KUFANYA USHIRIKINA

Written by mzalendoeditor
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 95 wa Kijiji cha Lwanzali kilichopo Lupembe Halmashauri ya Wilaya ya Njombe amekutwa ameuawa ndani ya nyumba yake huku upelelezi wa awali ukionesha kuwa chanzo ni kutokana na Mzee huyo kutuhumiwa kufanya ushirikina katika Familia yake.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema “Tumejaribu kwenda katika eneo lile na imebainika huyu Mzee walikuwa walikuwa wanamtuhumu kuwa anafaya mambo kishirikina katika Familia yake”
Kamanda Issah amesema Polisi wanaendelea kuchunguza ili kubaini ni nani aliyehusika na mauaji hayo ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

About the author

mzalendoeditor