Uncategorized

TIMU ZA ATLÉTICO DE MADRID, GETAFE FC NA REAL VALLADOLID ZIKO TAYARI KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

Written by mzalendoeditor

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Damas Ndumbaro (Mb), akiwa katika mkutano na uongozi wa timu ya Getafe inayoshiriki daraja la kwanza (Laliga) ya Uhispania. Kushoto kwa Mhe. Waziri, ni Mhe. Samwel W. Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi yake mjini Paris, Ufaransa.

Mhe. Waziri Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii (kushoto) akiwa na Mhe. Balozi Samwel W. Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi yake mjini Paris, Ufaransa, wakiwa wamesimama nyuma ya sanamu la mchezaji aliyevaa jezi inayoitangaza Tanzania

Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika mkutano na uongozi wa timu ya Atlético de Madrid.

………………………………………………….

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Damas Ndumbaro (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Samwel W. Shelukindo ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi yake mjini Paris, Ufaransa wamefanya mazungumzo na vilabu vya Atlético de Madrid na Getafe FC.

Vilabu hivyo vinashiriki ligi kuu ya Uhispania (Laliga), pia wamefanya mazungumzo na timu inayotarajia kupanda daraja ya Real Valladolid, inayomilikiwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Ronaldo De Lima.

Lengo la mazungumzo hayo, lilikuwa kushawishi timu hizo kuitangaza Tanzania kiutalii ili kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania.

Timu hizo ambazo zinaangaliwa na idadi kubwa ya watazamaji sio tu nchini Uhispania, bali pia duniani kwa ujumla, zimeonyesha utayari wa kuitangaza Tanzania kiutalii.

About the author

mzalendoeditor