BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko ya mchezo namba 144, kati ya Yanga na KMC zote kutoka Jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 10 na TPLB imeeleza mchezo huo utachezwa Machi 19 badala ya Machi 16 kama ilivyopangwa hapo awali huku sababu kubwa ikiwa ni kupisha marekebisho ya miundombinu ya Uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyopangwa kufanyika kuanzia Machi 15-18, 2022.

Katika hatua nyingine mchezo namba 142, wa Ligi Kuu Bara kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Simba uliopagwa kufanyika Machi 27, kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi umeahirishwa ili kupisha michezo ya kirafiki ya Taifa ya Tanzania ilipo kwenye kalenda ya FIFA.

Bodi hiyo imezitakia maandalizi mema ya michezo inayofuata klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu huu

Previous articleWAZIRI MKUU APOKEA MAJINA 453 YA AWALI WALIO TAYARI KUHAMA NGORONGORO
Next articleTIMU ZA ATLÉTICO DE MADRID, GETAFE FC NA REAL VALLADOLID ZIKO TAYARI KUUTANGAZA UTALII WA TANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here