Featured Kitaifa

MWANAMKE AONDOLEWA FIGO BILA KUJIJUA

Written by mzalendoeditor

Madaktari nchini Uganda wamethibitisha kuwa mwanamke aliyekuwa akifanya ya nyumbani nchini Saudi Arabia, aliondolewa figo yake ya kulia na sio ajali ya gari kama ilivyoarifiwa awali na mwajiri wake.

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imethibitisha hilo baada ya kupewa ripoti ya uchunguzi kutoka Hospitali kuu ya kitaifa ya Mulago.

Uchunguzi wa awali wa Polisi umetambua muajiri wake wa nchini Saudi Arabia kwa jina la Sadaffa Muhamed na alitoa ripoti bandia za kitabibu kuwadanganya wanafamilia ya muathiriwa.

Kufuatia taarifa hiyo ya uchunguzi sasa familia ya mwanamke huyo inaiomba serikali kusimamia suala hilo hadi haki itakapopatikana.

Judith Nakintu mwenye umri wa miaka 38 ana watoto watano na alichukuliwa na kampuni ya Nile Treasure Gate mnamo mwaka 2019 kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za nyumbani huko Jeddah nchini Saudi Arabia.

Baada ya kufanya kazi karibu miezi miwili, mawasiliano yake na familia yake yalikatika, ndipo mama yake mzazi alipoanza kufuatilia karibu miezi mitatu ndipo akaambiwa mwanae amepata ajali.

‘Alitufahamisha kwa simu kwamba alipata ajali nilikuwa nataka kufahamu familia yake, nikamuuuliza alipata ajali bila kampuni iliyompeleka kujua? Nikawapigia simu kampuni yake nikawaeleza, wakasema hawana habari wala taarifa’, alisema mama huyo.

Kampuni ya Nile Treasure Gate ilimpigia mama wa Nakintu simu…mnamo tarehe 30 Oktoba 2021. Mwanae alikuwa anatarajia kuwasili katika uwanja wa ndege wa Entebe siku hiyo. Aliondoka mpaka kwenye uwanja huo wa ndege kwa ajili ya kumpokea mwanae.

Alipowasili alimuona mwanae akiletwa kutoka kwenye ndege akiwa kwenye kiti cha wagonjwa cha magurudumu, hawezi kutembea na kuingizwa kwene gari la wagonjwa hadi Hospitali kuu ya Mulago.

CHANZO:BBCSWAHILI

About the author

mzalendoeditor