Featured Kitaifa

CHATANDA AWANADI ESTER MATIKO NA MWITA WAITARA WILAYANI TARIME

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wawanake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) awanadi na kuwaombea kura Wagombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Tarime Mjini Ester Matiko na Mwita Waitara wa Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, Leo Tarehe 10 Septemba, 2025, katika Muendelezo wa Kampeni ya kunadi Sera za Chama Cha Mapinduzi CCM Pamoja na kumuombea kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge pamoja na Madiwani.

Katika hatua nyingine Chatanda, amekemea vikali na kuwataka Wagombea na Wanachama wa CCM kuvunja Makundi yaliyopo Mkoani Humo haraka badala yake waelekeze nguvu zao zote katika kukitafutia Kura za kishindo Chama cha Mapinduzi kwa na Mgombea wake.

About the author

mzalendo