Na Ferdinand Shayo ,Manyara.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ,Exaud Kagahe ameipongeza Kampuni ya Mati Super Brands ambao ni wazalishaji wa vinywaji vikali kwa uwekezaji wa viwanda walioufanya pamoja na kushiriki kudhamini Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yanayoendelea katika viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mjini Babati Mkoani Manyara.
Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la kampuni ya Mati Super Brands Limited Naibu Waziri huyo amepongeza juhudi za kampuni hiyo katika kuwekeza na kulipa kodi Stahiki ya serikali.
Exaud amesema kampuni hiyo imekua mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka pamoja na kudhamini matukio mbali mbali ya kijamii na kiserikali.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited Elvis Peter amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kitaifa na kimataifa .
“Kampuni yetu imekua ni wadhamini wakuu wa Maonyesho ya Tanzanite Manyara TRADE FAIR ambayo yanakutanisha wafanyabishara kutoka ndani na nje ya nchi” Ameeleza Elvis.