Jumatatu, Novemba 23, 2026
HABARI MPYA
Michezo

CAS KUTOA UAMUZI WA MWISHO KESHO KUHUSU SAKATA LA UBINGWA WA AFCON

 

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Michezo-CAS inatarajia kutangaza uamuzi uliofikiwa na jopo hilo kuhusu bingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2025.

Hatua hiyo ya CAS inakuja baada ya Senegal kukata rufaa kupinga kunyang’anywa ubingwa wa AFCON na kupewa Morocco.

Mapema leo CAS iliwataarifu CAF, Senagal na Morocco kuwa uamuzi wa mwisho kuhusiana na sakata hilo utatolewa kesho.

Fainali ya AFCON kati wenyeji Morocco na Senegal ilikumbwa na sintofahamu dakika za mwisho wa mwisho kwa Senegal kugomea penati na kuamuru wachezaji kurejea vyumba vya kubadilishia nguo.

Baada ya majadiliano yaliyochukua zaidi ya dakika 15 hatimaye mchezo huo uliendelea ambapo Morocco walikosa penati kabla ya Senegal kuja kushinda mechi hiyo dakika za nyongeza na kutawadhwa mabingwa wa michuano hiyo.

Baada ya dakika 90 za uwanjani sakata hilo lilihamia nje ya uwanja kwa Morocco kukata rufaa CAF kupinga ushindi huo wa Senegal wakidai kuwa mchezo huo haukupaswa kuendelea baada ya wapinzania wao kugoma.

Baada ya Kamati ya Rufaa ya CAF kupitia malalamiko hayo iliamua kuwavua ubingwa Senegal na kuwapa Morocco.

Senegal waliamua kulipeleka sakati hilo CAS ambapo rufani yao ilisikilizwa mwezi uliopita na sasa inatarajiwa kutolewa maamuzi.