Featured • Kitaifa

TANZANIA, CHINA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI KUPITIA MPANGO WA BELT AND ROAD INITIATIVE

Written by Alex Sonna

 

Naibu Katibu Mkuu, Bi. Asha Khamis Abdulla akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), katika Jukwaa la Belt and Road Initiative lilifanyika sambamba na Mkutano wa Mwaka wa Financial Street Forum 2026, lenye lengo la kuimarisha uhusiano wa Kiuchumi, Biashara na Maendeleo ya Miundombinu kati ya China na nchi mbalimbali duniani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Argle Grand, Jijini Nairobi.

Naibu Katibu Mkuu, Bi. Asha Khamis Abdulla akifuatilia mojawapo ya mada zilizowasilishwa katika Jukwaa la Belt and Road Initiative lilifanyika sambamba na Mkutano wa Mwaka wa Financial Street Forum 2026, lenye lengo la kuimarisha uhusiano wa Kiuchumi, Biashara na Maendeleo ya Miundombinu kati ya China na nchi mbalimbali duniani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Argle Grand, Jijini Nairobi.

Naibu Katibu Mkuu, Bi. Asha Khamis Abdulla akisalimiana na Mhe. John Mbadi Ng’ongo Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango wa Kenya wakati wa Jukwaa la Belt and Road Initiative lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Argle Grand, Jijini Nairobi.

Naibu Katibu Mkuu, Bi. Asha Khamis Abdulla akiambatana na Balozi wa China nchini Kenya, Bi. Guo Haiyan kuelekea kwenye jukwaa Belt and Road Initiative lilifanyika sambamba na Mkutano wa Mwaka wa Financial Street Forum 2026, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Argle Grand, Jijini Nairobi.

Naibu Katibu Mkuu, Bi. Asha Khamis Abdulla akijadiliana jambo na Rais wa China Road and Bridge Corporation – Kenya office, Bw. YU Xiaodong Kabla ya jukwaa Belt and Road Initiative lilifanyika sambamba na Mkutano wa Mwaka wa Financial Street Forum 2026, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Argle Grand, Jijini Nairobi.

Kamishina msaidizi Idara ya Fedha za Nje – Wizara ya Fedha Bw. Melckzedk Daniel Mbise akifuatilia mojawapo ya mada zilizowasilishwa katika Jukwaa la Belt and Road Initiative lilifanyika sambamba na Mkutano wa Mwaka wa Financial Street Forum 2026, lenye lengo la kuimarisha uhusiano wa Kiuchumi, Biashara na Maendeleo ya Miundombinu kati ya China na nchi mbalimbali duniani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Argle Grand, Jijini Nairobi.

Naibu Katibu Mkuu, Bi. Asha Khamis Abdulla (Mwenye ushungi), Balozi wa China nchini Kenya, Bi. Guo Haiyan  wakiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali waliohudhuria Jukwaa la Belt and Road Initiative lilifanyika sambamba na Mkutano wa Mwaka wa Financial Street Forum 2026, lenye lengo la kuimarisha uhusiano wa Kiuchumi, Biashara na Maendeleo ya Miundombinu kati ya China na nchi mbalimbali duniani, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Argle Grand, Jijini Nairobi.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,WF – Nairobi)

Na. Ramadhani Kissimba, WF – Nairobi

Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na China kupitia Mpango wa Belt and Road Initiative (BRI), kwa kuendeleza miradi ya kimkakati katika sekta za usafiri, nishati, mawasiliano na miundombinu, inayolenga kukuza uchumi, kuongeza fursa za biashara na uwekezaji, pamoja na kuboresha maisha ya wananchi.

Akizungumza jijini Nairobi, Kenya, katika Jukwaa la Belt and Road Initiative, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Naibu Katibu Mkuu- Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla, alisema ushirikiano kati ya Tanzania na China umeendelea kufungua fursa za maendeleo katika miundombinu, biashara, uwekezaji na mageuzi ya viwanda.

Bi. Asha, alisema Tanzania inautambua Mpango wa Belt and Road Initiative kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kifedha kati ya nchi mbalimbali, huku ukichochea maendeleo endelevu na jumuishi yanayozingatia vipaumbele vya maendeleo ya taifa.

“Uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China, unaojengwa katika misingi ya kuheshimiana, kuaminiana na mshikamano, umeendelea kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya miundombinu, biashara, uwekezaji, nishati na mageuzi ya viwanda,” alisema Bi. Asha.

Bi. Asha, alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China pamoja na nchi nyingine duniani katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayolingana na vipaumbele vya taifa na malengo ya Dira 2050, ili kuongeza tija, kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi.

Katika hatua nyingine, Bi. Asha alieleza kuwa Tanzania, kwa kushirikiana na Zambia na China, inaendelea na mpango wa kufufua na kuboresha Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kupitia utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public-Private Partnership – PPP), ambapo kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuongeza ufanisi wa usafirishaji, kupunguza gharama za kusafirisha mizigo na kurahisisha biashara ya kikanda, hatua itakayochochea shughuli za kiuchumi na kuimarisha muunganiko wa masoko katika ukanda wa Kusini mwa Afrika.

“Uboreshaji wa reli ya TAZARA una umuhimu mkubwa katika kuimarisha muunganiko wa usafiri kati ya Tanzania, Zambia na eneo pana la Kusini mwa Afrika. Kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa zaidi za biashara na shughuli za kiuchumi katika ukanda huo,” aliongeza Bi. Asha.

Alieleza kuwa Tanzania inathamini ushirikiano unaoendelea na Serikali ya China pamoja na Benki ya Exim ya China katika kutekeleza miradi ya kipaumbele, ikiwemo upanuzi wa miundombinu ya usafirishaji wa umeme, mawasiliano vijijini, huduma za maji na mifumo endelevu ya usafiri mijini, miradi ambayo inasaidia katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za msingi, kuongeza fursa za kiuchumi na kusaidia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya Taifa.

Jukwaa la Belt and Road Initiative lilifanyika sambamba na Mkutano wa Mwaka wa Financial Street Forum 2026, uliotoa fursa ya majadiliano kuhusu ushirikiano wa kifedha, uwekezaji, miundombinu na maendeleo ya pamoja.

Tanzania na China zilisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano chini ya Mpango wa Belt and Road Initiative mwezi Septemba 2018, hatua iliyoweka msingi wa kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya maendeleo na kupitia ushirikiano huo, Tanzania inalenga kuendelea kuvutia uwekezaji, kuimarisha miundombinu ya kimkakati na kupanua fursa za biashara, sambamba na juhudi za kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kujenga uchumi imara na shindani.

About the author

Alex Sonna