Ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 , TANESCO Mkoa wa Dodoma, Oktoba 07,2026 imetoa elimu kwa wananchi wa Chang’ombe jijini Dodoma soko la Mavunde kuhusu matumizi ya nishati safi katika shughuli za kupikia.
Elimu hiyo imetolewa na Maafisa wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, ambao wameeleza kwa wananchi umuhimu na faida za kutumia nishati safi, pamoja na namna ya kutumia umeme kwa usalama na ufanisi wakati wa kupikia.
Takbribani wananchi zaidi ya 300 wamepata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu huduma za TANESCO, huku wakihimizwa kuendelea kutumia nishati safi katika shughuli zao za kila siku.
