Featured Kitaifa

MWONGOZO WA UKAGUZI WA MIFUMO KUIMARISHA UFANISI WA KAZI ZA UKAGUZI SERIKALINI.

Written by Alex Sonna


Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo ya Uelewa na Ugawaji wa Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa kwa Wakaguzi wa Ndani wa Serikali, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie (kushoto), akiagana na Mhasibu Mkuu wa Fungu 6 – Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Samwel Mangi, baada ya kumalizika kwa Mafunzo ya Uelewa na Ugawaji wa Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa kwa Wakaguzi wa Ndani wa Serikali, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie (kushoto), akijadiliana jambo na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Paison Mwamnyasi, wakati wa Mafunzo ya Uelewa na Ugawaji wa Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa kwa Wakaguzi wa Ndani wa Serikali, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi, Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bi. Vaileth Nyanga, akitoa wasilisho kuhusu muhtasari Mifumo ya Kuimarisha Ufanisi wa Kazi za Ukaguzi Serikalini, wakati wa program ya Mafunzo ya Uelewa na Ugawaji wa Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa kwa Wakaguzi wa Ndani wa Serikali, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, akigawa kitabu cha Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa kwa, Mkaguzi wa Ndani kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Bw. Ernest Josephat, mmoja wa washiriki wa program ya Uelewa na Ugawaji wa Mwongozo iliyowakutanisha wakaguzi wa ndani kutoka taasisi za umma ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Fedha, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie (katikati, walioketi), na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Paison Mwamnyasi (wa tatu kushoto, walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakaguzi wa Ndani baada ya Mafunzo ya Uelewa na Ugawaji wa Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa kwa Wakaguzi wa Ndani wa Serikali, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, WF – Dodoma)

Na. Asia Singano, WF – Dodoma.

Wizara ya Fedha imeendelea kuandaa na kuboresha miongozo mbalimbali inayolenga kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya ukaguzi na kuongeza ufanisi wa kazi hiyo, ili kuendelea kulinda fedha za umma na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, wakati akifungua Mafunzo ya Uelewa na Ugawaji wa Mwongozo wa Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa kwa Wakaguzi wa Ndani wa Serikali, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Mhandisi Nindie alisema kuwa mwongozo huo unahusisha hatua mbalimbali za mchakato wa ukaguzi, na kwamba baadhi ya vipengele vyake vinapitia hatua ya uhakiki ili kuhakikisha vinaendana na mahitaji na viwango vinavyotakiwa.

“Tunachukua baadhi ya vipengele kwa ajili ya kuvithibitisha, ambapo ni muhimu kupitia na kuthibitisha miongozo hiyo kabla ya kuanza kutumika kikamilifu. alisema Mhandisi Nindie.

Alieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa miongozo inayotumika katika kazi za ukaguzi ina ubora, inaeleweka na inawasaidia watendaji kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa watumishi kuwa na vyeti vya kitaaluma (certification), kwakuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuongeza ufanisi na ubora wa utekelezaji wa majukumu yao.

“Suala la kuwa na vyeti vya kitaaluma limekuwa sehemu muhimu ya mipango ya kuimarisha uwezo wa watumishi. Natambua kuwa tangu mwaka 2021 kulikuwa na mpango uliolenga kuongeza idadi ya watumishi wenye vyeti hivyo,” alisema Mhandisi Nindie.

Alibainisha kuwa kuendelea kuwekeza katika ujuzi na taaluma za watumishi ni hatua muhimu katika kuboresha utendaji kazi na kuhakikisha majukumu ya taasisi yanatekelezwa kwa viwango vinavyohitajika.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na Wizara ya Fedha, kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali yakiwakutanisha Wakaguzi wa Ndani kutoka taasisi za umma na kutoka Wizara ya Fedha, ili kuwaongezea uelewa katika utekelezaji wa majukumu yao.

About the author

Alex Sonna