Featured Kitaifa

DKT.MPANGO: TANZANIA BADO INALIA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango , akizungumza  wakati akifungua Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza Hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk. Ashatu Kijaji, akizungumza wakati wa Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya jitihada za uhifadhi wa mazingira kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) wakati wa Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika jijini Dodoma.

Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapongeza Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mnadan ya mkoani Dodoma mara baada ya kuimba wimbo wa kuhamasisha utunzaji mazingira katika Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango , akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna_DODOMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Philip Mpango amesema licha ya jitihada zinazofanywa na serikali kuondokana na uharibifu wa mazingira lakini bado Tanzania inalia hali ya mazingira sio nzuri.

Kutokana na hali hiyo, Dkt.Mpango amewataka viongozi na wadau katika mkutano maalum wa hali ya mazingira nchini unaofanyika jijini Dodoma kujadili taarifa ya nne ya mazingira ambayo imebainisha masuala mbalimbali ikiwamo ongezeko la uharibifu wa misitu.

Dkt.Mpango amesema kwa kiasi kikubwa athari za mazingira zinatokana na tabiawatu ikiwemo ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa misitu,kilimo kisicho endelevu na ufugaji holela usiozingatia uwiano wa idadi ya mifugo na maeneo ya malisho .

“Mambo mengine yanayochangia uharibifu wa mazingira ni pamoja na utupaji taka ovyo, uharibifu wa vyanzo vya maji,uvamizi wa ardhi pamoja na matumizi ya Nishati Chafu.”amesema Dkt.Mpango

Aidha amefafanua kuwa yapo mambo mbalimbali yanayochangia hali mbaya ya mazingira nchini ikiwemo Sheria Kinzani kama vile Mkaa kuwa chanzo cha mapato cha Wakala wa Misitu(TFS) hii inahamasisha utoaji wa vibali vya kukata miti.

Pia ameongeza kuwa vitalu vichache vya miti,miti inayopandwa kutotunzwa,kutotosheleza kwa miundombinu ya ukusanyaji na uhifadhi wa taka,uchache wa viwanda vya kurejeleza taka pamoja na gharama za Teknolojia ya kijani.

Dk.Mpango amesema Serikali imeendelea kukabiliana na uharibifu wa mazingira ni pamoja na kuandaa Sera,kanuni, pamoja na upandaji miti, kampeni za usafi hasa mjini na kwenye fukwe na kuhamasisha utunzaji wa mazingira kupitia vyombo vya habari.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk. Ashatu Kijaji, amesema kupitia mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwamo ya biashara ya kaboni na inatarajiwa kuongeza hamasa ya uwajibikaji katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar, Harusi Said Suleiman, amesema Zanzibar imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi kwenye mazingira na Agosti 17, mwaka huu walizindua program ya kuirudisha Zanzibar ya kijani.

About the author

mzalendoeditor