Featured Kitaifa

PROF. MKUMBO; SERIKALI HAITAKUWA KIKWAZO KWA AZAKI

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa ,Kitila  Mkumbo akizngumza wakati akifungua Wiki ya AZAKI iliyoanza rasmi leo Septemba 9-13, 2024 Jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation For Civil Society  FCS – Justice Rutenge, akizunguza lipokuwa akitoa hotuba yake ya utanguliza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya AZAKI , Jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkazi wa Trademark Africa Elibariki Shammy, akizungumza katika mkutano huo.

PICHA NA; FCS

Na; Hughes Dugilo, ARUSHA.

Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa, Kitila  Mkumbo amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia nchini nakwamba haitakuwa kikwazo kwao katika shughuli zake za kuleta maendeleo, sanjari na kutoa mawazo yatakayojenga zaidi ili kutafuta fursa zilizopo ndani na nje ya nchi.

Profesa Mkumbo amesema hayo wakati akifungua Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) iliyoanza rasmi leo Septemba 9, 2024 jijini Arusha.

Profesa Mkumbo amsema ni vema sasa Asasi za Kiraia zikashirikiana na serikali katika kutoa maoni yao ikiwemo kukaa meza moja kutaua changamoto zinazoibuka sanjari na kutafuta fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi katika kukuza uchumi

Prof. Mkumbo amesema, lengo kuu la serikali ni kuhakikisha ustawi wa watu wote  unakuwa, na ili kufika huko ni  vema zaidi kujifunza kupitia kwa watu, kuwa wabunifu na kutoa maoni  katika kuhakikisha Dira ya Mendeleo ya Taifa ya mwaka 2050  inaleta tija zaidi hususan katika uwekezaji kwenye elimu, miundombinu ikiwemo umeme wa uhakika.

‘’AZAKI zihakikishe zinaisemea jamii  changamoto ambazo wanaziona na kutatuliwa ili kuisaidia serikali kuzishughulikia na si kuilalamikia kuwa haifanyi kazi ilihali hawajazibainisha ili zifanyiwe kazi na jamii iweze kupata mabadiliko’’. Amesema Mkumbo.

Amesema nchi zilizoendelea zimepiga hatua katika maendeleo kwa sababu ya umeme hivyo uwepo wa Bwawa la mwalimu Nyerere  nchini Tanzania hadi kukamilika kwake utawezesha umeme kupatikana kwa wingi ikiwemo uchumi kukua kupitia viwanda vinavyozalisha bidhaa ndani ya nchi  na kuuza  bidhaa hizo nje ya nchi kwakushirikiana na sekta binafsi hususan za kilimo .

Naye rais wa Foundation For Civil Society (FCS), Dk Stigmata Tenga amesisita kuwa lazima mabadiliko ya watanzania yatokee kupitia AZAKI ambazo ndio husemea wananchi wenye changamoto mbalimbali katika sekta za afya ,elimu, miundombinu ya barabara ikiwemo utoaji wa fursa za fedha kupitia taasisi mbalimbali zinazowawezesha wananchi kujikwamua kimaisha kupitia mikopo yenye riba nafuu na kuongeza kuwa rasilimali watu ni muhimu kuzingatiwa katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Africa Elibariki Shammy  amesema   mkakati wa serikali ni kuhakikisha biashara za kidigitali zinakua zaidi kwa kushirikisha vijana kwa kasi kubwa kupitia biashara kwa kuwawekea mazingira rafiki yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo nchini.

Awali Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Isabelle Mignucci ameshukuru ushikiano kati ya serikali ya Tanzania na mashirika mbalimbali unaoleta tija katika maendeleo sanjari na kuhakikisha vijana wanapata fursa za maendeleo kupitia teknolojia na ubunifu unaoleta tija  zaidi katika ukuaji wa uchumi.

Mwisho.

Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Isabelle Mignucc akizunguza alipokuwa akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo Jijini Arusha.

About the author

mzalendoeditor