Featured Michezo

MICHUANO YA ALL AFRICAN GAME 2023 YAANZA KUTIMUA VUMBI NCHINI GHANA.

Written by mzalendo

Mashindano ya Afrika (All African Games 2023) yamezinduliwa rasmi Machi 8, 2024 Jijini Accra, Ghana yakiongozwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Nana Akufo Addo, huku yakishuhudiwa na Wanamichezo kutoka Mataifa 54 ikiwemo Tanzania na kupambwa na maandamano pamoja na burudani mbalimbali.  

Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na washiriki Zaidi ya 8000 wakijumuisha wachezaji, Maafisa, madaktari wa timu pamoja washangiliaji ambapo michezo mbalimbali inatarajia kuchezwa katika viwanja tofauti kuanzia Machi 8 hadi 23, 2024.

Katika Mashindano hayo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameongoza timu ya wanamichezo kutoka Tanzania watakaochuana na wachezaji wa mataifa mengine katika mchezo wa Kriketi Wanawake, Mpira wa Miguu Wanawake chini ya miaka 20, Judo, Riadha, kuendesha baiskeli na kuogelea.

About the author

mzalendo