Kimataifa

UTURUKI KUTAFUTA MAFUTA NA GESI SOMALIA

Written by mzalendo

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) akipeana mkono na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud Aprili 23, 2015. Picha na ofisi ya habari ya rais wa Ururuki.

*********************************************

Kulingana na maafisa wa nchi zote za Somalia na Uturuki wamesema nchi hizo mbili zimetia saini makubaliano ya kutafuta mafuta na gesi ambayo yataimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Petroli na mali asili wa Somalia, Abdirizak Mohamed amesema chini ya makubaliano yaliyosaininiwa Alhamisi nchini Uturuki ni kuboresha maendeleo ya pande mbili , kisayansi, kiteknolojia na ushirikiano wa kibiashara kati ya Uturuki na Somalia katika kuendeleza mafuta na gesi ya nchi yake.

Mohamed amesema Uturuki itatafuta mafuta na gesi nchini Somalia, kote ufukweni na baharini.

Amesema mpango huo ni moja ya itifaki za Mkataba wa Mfumo wa Ushirikiano wa Kiuchumi uliofikiwa na nchi hizo mbili mwezi uliopita.

Chini ya makubaliano hayo, ambayo yatadumu kwa miaka 10, Uturuki itajenga, kutoa mafunzo na kilipatia vifaa jeshi la wanamaji la Somalia, kulingana na waziri mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre.

Waziri huyo wa petroli na mali ya asili amesema mkataba utakaofuata utakuwa na maelezo ya kushirikiana uzalishaji pamoja na ratiba ya makubaliano.

About the author

mzalendo