Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema Jeshi la Kujenga Taifa limeachana na matumizi ya mkaa na kuni katika kuandaa chakula cha vijana katika makambi ya JKT.
Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo leo Juni 15, 2026 katika kikosi cha Ruvu JKT Mkoani Pwani wakati akifungua Mafunzo ya vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Linda Amani.
Amesema katika kuunga mkono juhudi za serikali za utunzaji wa mazingira, vikosi na makambi ya JKT vimewezeshwa kutumia majiko ya gesi na mkaa mbadala unaotengenezwa na wanakikosi kwa kutumia mabaki ya mimea katika vikosi hivyo.
