Featured Michezo

YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI CAFCL

Written by mzalendo

TIMU ya Yanga SC imeandika historia ya kufuzu hatua ya robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya  CR Belouizdad ya Algeria mchezo wa hatua ya Makundi uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 43,Stephane Aziz Ki dakika ya 46,Kennedy Musonda dakika ya 48 na Joseph Guede dakika ya 84.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 8 huku Al Ahly wakiwa na Pointi 9 ,nafasi ya tatu CR Belouizdad Pointi 5,Medeama Pointi 4 mchezo wa mwisho Yanga itasafirisha kwenda Misri kucheza na Al Ahly.

Yanga SC imefuzu moja kwa moja kwa kuwa Mbabe wa ‘head to head’ kati yake na CR Belouizdad kwa maana hata kama CR Belouizdad atashinda mechi yake ya mwisho hawezi kufuzu.

Itakumbukwa mechi ya kwanza Yanga ilifungwa mabao 3-0 kabla ya leo kushinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa marudiano.

About the author

mzalendo