Kitaifa

AJALI ILIYOUA WATU 15 RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE ARUSHA

Written by mzalendo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali iliyotokea Mkoani Arusha.
Rais Samia ameandika ‘Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya watu 15
katika ajali iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, mkoani Arusha.
Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waliopoteza jamaa zao katika katika ajali hii’
‘Ajali hizi zinachukuwa wapendwa wetu, nguvu kazi ya Taifa na mihimili ya familia. Naendelea kutoa wito kwa kila mmoja kuzingatia sheria za usalama barabarani katika matumizi ya vyombo vya moto.
Naagiza vyombo vyetu vya ulinzi, usalama na udhibiti kuendelea kuhakikisha vinasimamia sheria kikamilifu, ikiwemo ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya usafiri na udhibiti wa leseni kwa madereva wanaorudia kuvunja sheria mara nyingi na wakati mwingine kusababisha watu kupoteza maisha’
‘Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina’. – Rais Samia.

About the author

mzalendo