Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa,akizungumza wakati akifungua   kikao kazi cha Maofisa Utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali kilichofanyika leo Februari 2,2024 jijni Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt Charles Msonde,akizungumza wakati wa  kikao kazi cha Maofisa Utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali kilichofanyika leo Februari 2,2024 jijni Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Denis Londo,akizungumza wakati wa  kikao kazi cha Maofisa Utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali kilichofanyika leo Februari 2,2024 jijni Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani),wakati akifungua   kikao kazi cha Maofisa Utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali kilichofanyika leo Februari 2,2024 jijni Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mara baada ya kufungua   kikao kazi cha Maofisa Utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali kilichofanyika leo Februari 2,2024 jijni Dodoma.

Na.Alex Sonna,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amefungua kikao kazi cha Maofisa Utumishi wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali wanaohakiki kwa kina changamoto za walimu hususan upandishwaji wa vyeo.

Akifungua leo Februari 3, 2024 kikao hicho jijini Dodoma, Waziri Mchengerwa amesema katika kuhakikisha kuwa malalamiko ya Walimu yanashughulikiwa, Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais UTUMISHI iliagiza Tume ya Utumishi wa Walimu kufanya uchambuzi na kubaini walimu wote wenye changamoto katika upandaji wao wa vyeo.

“Niwapongeze Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kazi nzuri ambayo wameifanya ambapo uchambuzi umefanyika na walimu zaidi ya 136,000 wamebainishwa kuwa na changamoto,
pamoja na kazi nzuri iliyofanyika, kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa malalamiko ya walimu wote yanashughulikiwa kwa ufanisi, nimeelekeza uhakiki wa kina ufanyike kwa kuhusisha taarifa za watumishi kama zilivyo kwenye Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara (HCMIS),” amesema

Ameagiza kushughulikia kikamilifu changamoto hizo ndani ya siku 14 na kufanya kazi hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuhakikisha hakuna Mwalimu anayeachwa baada ya zoezi hilo kufanyika.

Wakati huohuo, Waziri Mchengerwa amewakumbusha Waajiri na Mamlaka zote zinazohudumia Walimu kusimamia vyema maslahi ya walimu ikiwa ni pamoja na kutatua kero walizo nazo.

“Naomba niweke wazi mimi sitamvumilia mtendaji yeyote ambaye hawajibiki kushughulikia kero za walimu na vilevile sitamani kusikia walimu wana malalamiko kuhusu maslahi yao ya kiutumishi,”amesema.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt Charles Msonde,amesema wameamua kufanya kikao kazi cha siku 14 cha maafisa utumishi wa halmashauri ili kuhakiki taarifa za walimu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Denis Londo ,ameipongeza kazi kubwa iliyofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia ya kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu.

Previous articleRC MNDEME ATAKA POLISI WAONGEZE KASI KUDHIBITI AJALI NA WANAOJIUZA
Next articleSERIKALI YAJA NA SULUHISHO LA KUDUMU NJIA YA RELI YA KATI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here