Featured Kitaifa

WIZARA YA AFYA KUJIKITA KATIKA UBORA WA HUDUMA

Written by mzalendo

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akizungumza wakati akifungua   Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (hayupo pichani),wakati akifungua   Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.

Mtaalamu wa Ubora wa Huduma kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF)  Bi.Shally Zumba Mwashemele,akizungumza wakati wa  Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Dkt.Saturini Manangwa ,akizungumza wakati wa  Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.

Msajili wa Baraza la Madaktari Dkt. David Poul,akizungumza wakati wa  Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.

Msajili wa Baraza la Wauguzi,Bi.Agness Mtawa,akizungumza wakati wa  Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.

Na.Nestory James-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya  imesema itajikita katika ubora wa huduma kwa Wateja  kwa manufaa ya wananchi huku ikiwataka watumishi wa afya kuzingatia maadili ya kazi zao.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ameyasema hayo leo Januari 10,2024 Jijini Dodoma,wakati wa Mkutano wa  kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora  kuanzia ngazi ya  awali  kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar.

Maghembe amesema kuwa Sekta ya afya ni sekta ambayo inagusa Maisha ya watu hivyo maboresho makubwa yamefanywa na Rais  katika sektaya afya  hivyo ni muhimu watumishi wa sekta ya afya kubadilisha mitazamo yao katika kufanya ubora wa huduma kwa wateja.

“Napenda tu niwahakikishie watanzania kuwa maboresho makubwa yaliyofanyika yataenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa ngazi zote,” Amesema Dkt.Maghembe

Aidha Naibu Katibu Mkuu,amebainisha kuwa Watoaji wa huduma wakibadilisha  mitazamo yao katika syuala la ubora wa huduma wananchi watafurahia huduma wanazozipata kwakuzingatia maadili,utu heshima na huruma ili maboresho yaliyofanyika yaendane na utoaji wa huduma kwa wananchi ili waweze kufurahia huduma za  afya.

Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Madaktari Dkt. David Poul  ameeleza suala la utoaji wa huduma kwa mteja katika taaluma ya afya ni muhimu ambalo lina hitaji kuzingatia  misingi na   heshima inayostahiki kwa wananchi.

Amesema mteja ndio sehemu ya huduma ya heshima ndani ya taaluma za afya wnaangalia waweke mikakati gani hasa kwakuendana na muiongozo na maadili yaliyopo ndani ya taaluma ili kutoa huduma bora.

“Kumuhudumia mteja nikumuangalia yeye na hali yake na kumfanya mteja aondoke eneo la huduma akiwa ameridhika”,Amesisitiza Dkt.David

Awali Msajili wa Baraza la Wauguzi,Agness Mtawa   amesema kuwa watayafanyia akzi  maagizo waliyopewa katika utoaji wa huduma bora kwa wateja katika utendaji kazi wao.

About the author

mzalendo