MWANDISHI WETU.


KATIKA
kuadhimisha Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mamlaka ya
Masoko ya Mitaji ya dhamana (CMSA) imetinga visiwani humo kutoa elimu
juu ya masuala ya Uwekezaji katika Masoko ya mitaji.

Maonyesho
hayo ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar ambayo yanafanyika Dimani
Fumba visiwani humo yameanza rasmi Januari 7, mwaka huu ambapo
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ally Mwinyi, atakuwa mgeni rasmi.

Akizungumza
na wanahabari, Afisa uhusiano na elimu kwa umma, Stella Anastazi
amesema, lengo kuu la kuja katika maonyesho hayo ni kutoa elimu juu ya
masoko ya mitaji.

Stella amesema amefurahi kuona muitikio mzuri na mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali waliotembelea banda la CMSA ili kujifunza.

 
“Nia
na madhumuni ni kuleta elimu hii kwa wananchi wa Zanzibar, na pia
kuwajuza maendeleo makubwa ambayo mamlaka imekuwa nayo mpaka sasa,”
Amesema
imekuwa fursa kubwa kukutana na watu ambao wanaelimu juu ya mitaji
hivyo hata kuwapa madini ya uwekezaji imekuwa rahisi tofauti na kukutana
na mtu asiye na elimu ya masoko hayo.


Aidha
Stella amesema ni wakati muafaka kwa wawekezaji kuwekeza kwani wao
wanatoa ushauri zaidi na kujibu sintofahamu ambazo wananchi wamekuwa
wakizipitia katika uwekezaji.


“Tumekuja
na vipeperushi vingi vitazidi kumpa elimu muhusika ili kujua mambo
mengi yanayohusu mitaji na masoko kupitia hivi vipeperushi pia vinampa
mwongozo wa namna gani ya kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja
na mambo mengi yanayofanyika CMSA,”amesema.

Aidha amewataka Watanzania kuwekeza ili kupata ongezeko la thamani ambayo ni faida kubwa sana kwao.

“Tuna
kipeperushi kinacho toa elimu ya kujiepusha na uwekezaji wa upatu
haramu ambao sio mzuri kwao maana akikosea anaweza kuchukuliwa hatua za
kisheria maana kuvunja sheria ya nchi ni kosa la jinai kufanya kosa
hilo”amesema Stella.

Mmoja wa wananchi kisiwani Zanzibar Hamis
Shaibu Hamad,amesema alikuwa akisikia mamlaka ya masoko ya mitaji lakini
hakufahamu ni vitu gani vizuri vinapatikana huko ila baada ya
kutembelea banda amefarijika kufahamu mengi.

“Unajua ukiwa
haujapata elimu ya kitu husika unaweza kujikosesha fursa lakini mimi
nimepata vitu vizuri kabisa kutika katika hili banda la CMSA nitakuwa
balozi mzuri kwa wenzangu huko ili na wao waweze kuwekeza zaidi,”alisema
Hamad.

Afisa
uhusiano na elimu kwa umma kutoka CMSA, Stella Anastazi,akitoa elimu ya
uwekezaji kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo
katika maonesho ya biashara Zanzibar ( Zanzibar International Trade
Fair)

Previous articleWIZARA YA AFYA KUJIKITA KATIKA UBORA WA HUDUMA
Next articleWAGONJWA 6,931 KUTOKA NJE YA NCHI WALITIBIWA TANZANIA, MWAKA 2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here