Featured Kitaifa

WAZIRI JAFO AMWAKILISHA RAIS SAMIA TANZANIA DAY DUBAI

Written by mzalendo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisoma hotuba kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Siku ya Mtanzania) yaliyofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Luteni Jenerali (Mstaafu) Yacoub Hassan Mohamed wakati wa Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Siku ya Mtanzania) yaliyofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Viongozi wa Diaspora kabla ya kusoma hotuba kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Siku ya Mtanzania) yaliyofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.

………….

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru (Siku ya Mtanzania) yaliyofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE.

Katika hotuba aliyoisoma kwa niaba ya Rais Samia, Waziri Jafo amesema Serikali inatambua mchango na umuhimu wa Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) katika kuleta maendeleo nchini Tanzania.

Amesema tayari Serikali imechukua hatua ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano kwenye kazi na ajira uliosainiwa katika kipindi cha Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) unaoendelea.

Hivyo, amesema hatua hiyo itasaidia katika kutatua changamoto nyingi zilizokuwepo za wafanyakazi hasa wa majumbani na wote kwa ujumla watakuwa katika mazingira mazuri ya kisheria kwa pande zote mbili.

Waziri Jafo amesema hatua hizo za makusudi ni mojawapo ya mikakati ya Serikali katika kuhakikisha Diaspora wanawekewa mazingira wezeshi ya kuwatambua kisera na hatimae kisheria. 

Dkt. Jafo amesema kuwa Rasimu ya Sera ya Mambo ya Nje iko katika hatua za mwisho chini ya uratibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo imewatambua.

Amesema katika Sera hiyo mpya kutakuwa na kipengele maalumu cha Diaspora ambapo Serikali imeanza na mkakati ya kuwawekea hadhi maalumu Watanzania hao.

“Ni mategemeo ya Serikali kuwa Diaspora mtakuwa na upendeleo maalumu ikiwa ni pamoja na kuweza kurudi Tanzania kirahisi na kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kichumi tofauti na wageni kwani katika kipindi chote cha historia, uhusiano kati ya Tanzania na UAE umekuwa wa kipekee,“ amesema Dkt. Jafo. 

Aidha, Dkt. Jafo ameongeza kuwa yapo mafanikio mengi yakiwemo ushirikiano wa kibiashara, utamaduni na maendeleo ya kijamii na ili kuendelea kunufaika na fursa zilizopo katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kupitia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili.

 

Kwa upande mwingine amesema Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imezindua mfumo wa mawasiliano na Diaspora wake kote duniani uitwao Diaspora Digital Hub System (DDH) ambao utasaidia usajili wa wanadiaspora wa makundi yote kwa lengo la kuwatambua na kuwaweka katika mfumo maalum ili iwe rahisi kwa mawasiliano na kuwaunganisha katika mitandao ya huduma muhimu.

 

​ 

About the author

mzalendo