Featured Kitaifa

MAHAFALI YA 34 YA TAASISI YA SANAA BAGAMOYO YAFANA SERIKALI YAAHIDI NEEMA

Written by mzalendo

SERIKALI imejipanga kuhakikisha inaboresha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Cha Malya, kuhakikisha zinatoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi wenye vipaji nchini.


Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinyijuma wakati wa mahafali ya 34 ya TaSUBa yaliyofanyika katika viwanja vya taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, alisisitiza kwamba serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia katika taasisi hizo zilizopo chini ya wizara yake.

Alisema taasisi hizo zimekuwa na mchango mkubwa wa kuibua vipaji vya vijana ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasanii na wanamichezo na kujitengenezea ajira kupitia vipaji vyao.

“Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia, itaendelea kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia katika taasisi ya TaSUBa na Chuo Cha Malya, lengo ni kuhakikisha zinafikia malengo ya kutoa mafunzo kwa vijana wengi zaidi katika sekta ya sanaa na michezo.

“Matokeo ya uwekezaji huu unaofanywa na serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha tunaimarisha na kuongeza ubora wa mafunzo yanayotolewa na pia kutoa nafasi zaidi kwa vijana wenye vipaji vya sanaa na michezo,” alisema.

Pia Naibu Waziri alisisitiza kwamba ana mpango wa kubalisha sheria na kanuni za vyama na mashirikisho ya sanaa, kuhakikisha kila atayekuwa anataka kugombea nafasi ya uongozi katika soko la sanaa awe amesoma angalau kozi fupi TaSUBa.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya TaSUBa, Dkt. Herbert Makoye alisema jumla ya wanafunzi 270 walihitimu katika fani mbalimbali ambapo astashahada walikuwa 158 na stashahada wahitimu 112.

Alisema wanaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwapa fedha za maendeleo ambazo zimeiwezesha taasisi hiyo kufanya ukarabati wa baadhi ya majengo na kununua vifaa vya kufundishia.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutupatia fedha za maendeleo ambazo zimeiwezesha taasisi kufanya ukarabati wa baadhi ya majengo na kununua vifaa vya kisasa vya kufundishia.

“Tupo katika mchakato wa kuanzisha televisheni na redio yetu kwa ajili ya kupanua wigo wa mafunzo kwa wanafunzi mbalimbali,” alisema Dk. Makoye.

Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, akizungumza wakati wa mahafali ya 34 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), ambapo aliwataka wahitimu wakaitumie elimu waliyoipata kuifanya sanaa kuwa ajira kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, akimkabidhi cheti staa wa muzuki wa hip hop Farid Kubanda ‘Fid Q’ baada ya kuhitimu kozi fupi ya Mafunzo ya utawala na Masoko katika sanaa katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), wakati wa mahafali yaliyofanyika mwsihoni mwa wiki katika taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’,akimkabidhi cheti Rachel Benjamin baada ya kuhitimu elimu ya Sanaa ngazi ya cheti katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), wakati wa mahafali yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani PwaniNaibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’,aki akimkabidhi cheti kwa Nemes Stephen baada ya kuhitimu elimu ya Sanaa ngazi ya cheti katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), wakati wa mahafali yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’,akimkabidhi cheti Daniel Leonard baada ya kuhitimu elimu ya Sanaa ngazi ya cheti katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), wakati wa mahafali yaliyofanyika mwishoni mwa katika taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya wanachuo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) akizungumza Kwa niaba ya wanafunzi wa chuo hicho wakati wa mahafali ya 34 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkuu wa chuo Cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), Dkt.Herbert Makoye akizungumza wakati wa mahafali ya 34 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa katika taasisi hiyo, Bagamoyo mkoani Pwani.

Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ akifurahia jambo na mwenyeji wake Mkuu wa chuo Cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), Dkt. Herbert Makoye

Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikitoa burudani wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi hiyo.Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikitoa burudani wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi hiyo.

About the author

mzalendo