MABINGWA Mara 29 Tanzania bara Timu ya Yanga imevuna kiasi cha Shilingi 7 bilioni kwa mwaka kutokana na wadhamini mbalimbali wa timu hiyo.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 24,2023 jijini Dar es Salaam na Rais wa Yanga Mhandisi Hersi Said wakati wa mkutano mkuu wa klabu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC)
Rais Said amesema kuwa kiasi hicho kimepatikana kwa msimu wa 2022/23 uliomalizika hivi karibuni.
“Tunawashukuru na kujivunia sana wadhamini wetu kwa sababu katika michezo mbalimbali tumetumia gharama nyingi hivyo tunajivunia uwepo wao,” amesema
Amewataja wadhamini hao SportPesa, Azam TV na Kampuni ya Haier inayojihusisha na usambazaji na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya ofisini na majumbani, ila Yanga imepata Sh3.5 bilioni kwa mwaka kutokana na ushiriki wao katika mashindano mbalimbali.