Featured Kitaifa

RC SENYAMULE -MIRADI YOTE IKAMILIKE KABLA YA MWISHO WA MWAKA WA FEDHA 

Written by mzalendoeditor

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo katika kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa miradi inayotakiwa kukamilika ifikapo Juni 30/2023. Kikao hicho kimefanyika jana tarehe 25/05/2023 katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi yake jengo la Mkapa.

Wakuu wa Wilaya za Mpwapwa Sophia Kizigo (katikati), Chamwino Gift Msuya (kulia) na Kongwa Remidius Mwema (kushoto) waliposhiriki kikao kazi cha kupitia Utekelezaji wa Miradi inayotakiwa kukamilika kabla ya kumalizika kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/2023 kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jengo la Mkapa.

Katibu Tawala Msaidi (Mipango na Uratihu) Mkoa wa Dodoma Bw. Charles Mduma akiwasilisha Taarifa za Fedha, Mipango na matumizi ya Fedha za Miradi mbalimbali kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/2023 unaomalizika Juni 30/2023 katika kikao kazi cha kupitia Utekelezaji wa Miradi mbalimbali kilichofanyika 25/05/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo jengo la Mkapa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewataka  Wakurugenzi na
Wakuu wa Wilaya za Dodoma kukamilisha miradi yote kwa wakati  kabla ya kukamilika
mwaka wa fedha wa 2022/2023 ambao utafikia tamati ifikapo Juni 30, 2023.
Senyamule ametoa maagizo hayo leo Mei 25, 2023 alipofanya kikao kazi na viongozi
wa Halmshauri za Wilaya na Mji za Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa mikutano wa
Ofisi yake.
"Tumebakiwa na takribani mwezi mmoja wa kukamilisha miradi yote kwa muda
uliowekwa tunatakiwa kufanya haraka na kwa weledi kabla ya Juni 30, kwakuwa Mhe.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatafuta fedha kwa kasi kwahiyo na sisi aliotuteua
kumsaidia tunatakiwa tufanye kazi kwa nguvu ili kumuunga mkono.
"Lazima tufanye ubunifu ili majengo ya miradi tuliyopatiwa fedha yakamilike kwa wakati
na niwasisitize muwalipe mafundi fedha zao kwa wakati kwasababu ukishamlipa fundi
atafanya kazi kwa weledi, vilevile tununue vifaa kwa wakati ili kuondoa ucheleweshaji
wa namna yoyote ili iwe ikiwa ni pamoja na kuwakwamisha kuendelea na kazi zao kwa
mujibu wa mpango kazi uliopo", Amesema Senyamule 
Aidha amewaasa viongozi hao wa Wilaya kufanya uchambuzi wa vyanzo vyote
ambavyo havikukusanya mapato na kuvitafutia namna nzuri ya kukusanya mapato na
amebainisha kuwa Mkoa umekusanya mapato kwa asilimia 76 huku asilimia 24 pekee
zikisali. Senyamule amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji na Wilaya

About the author

mzalendoeditor