Featured Michezo

SIMBA SC YATUPWA NJE KOMBE LA ASFC

Written by mzalendoeditor

HAUKUWA Msimu wa Mafanikio kwa Simba SC ndivyo unaweza kusema! baada ya kutupwa nje kwa mbao 2-1 na Azam FC katika hatua ya Nusu Fainali Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) mchezo uliopigwa uwanja wa  Nangwanda mkoani Mtwara.

Azam FC walianza kupata bao dakika ya 22 likifungwa na Lusajo Mwaikenda baada ya mlinda mlango wa Simba SC kuutema Mpira hata hivyo bao hilo halikudumu kiungo Mkabaji  Sadio Kanout aliisawazishia Simba SC  dakika ya 28  na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko hayo yaliinufainsha Azam FC mnamo dakika ya 74 Prince Dube alipachika bao la ushindi.

Kwa Matokeo hayo Azam FC imetinga Fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2023 na sasa inasubiri Mshindi Kati ya Singida Big Stars au Yanga SC Fainali itkayopigwa uwanja wa  Mkwakwani Tanga.

About the author

mzalendoeditor