Featured Kitaifa

MKUU WA JKT AHITIMISHA MAFUNZO YA VIJANA, OP JENERALI VENANCE MABEYO KATIKA KIKOSI CHA RWAMKOMA JKT, MARA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa kuendesha Mafunzo ya Vijana wa Kitanzania

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo wakati akihitimisha Mafunzo ya Awali ya Kijeshi kwa Vijana wa Kujitolea Operesheni Jenerali Venance Mabeyo katika kikosi cha Rwamkoma JKT mkoani Mara.

Sanjari na Hilo, Amewasihi Vijana hao kutunza afya zao pamoja na kujiepusha na matumizi ya Madawa ya kulevya

Nae Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) amewapongeza Vijana hao kwa kuitimu mafunzo yao na kuwataka kwenda kukiishi kiapo chao

Akimkaribisha Mkuu wa JKT kutoa nasaha na kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT Kanali Aisha Matanza amesema, Vijana hao wamewawakilisha Vijana wenzao katika makambi yote yaliyoendesha Mafunzo hayo.

Akitoa taarifa ya Mafunzo, Kamanda Kikosi cha Rwamkoma JKT, Luteni Kanali Gaudencia Mapunda amesema

Vijana wa Kujitolea Operesheni Jenerali Venance Mabeyo yalifunguliwa Novemba 28, 2022 katika Makambi ya JKT yaliyoendesha Mafunzo hayo yalliyochukua majuma 16 ambapo yalianza kuhitimishwa kwa tarehe tofauti kuanzia Machi 7, 2023 hadi leo hii Machi 17,2023 Mkuu wa JKT amefunga zoezi la uhitimishwaji wa mafunzo hayo.

About the author

mzalendoeditor