Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATETA NA RAIS WA KAMPUNI YA SSRT YA NCHINI KOREA IKULU CHAMWINO DODOMA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kampuni ya Utengenezaji wa Mabehewa ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRT) ya Nchini Korea Bw. Gye Shul Park aliyeambatana na Ujumbe wake uliofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 02 Febuari, 2023. Rais wa Kampuni hiyo ameonesha nia ya kujenga Kiwanda cha kuunga Mabehewa hapa nchini, ambayo itaweza kuleta ajira kwa Watanzania, kuongeza Pato la Taifa na pia kuzinufaisha nchi jirani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya Utengenezaji wa Mabehewa ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRT) ya Nchini Korea Bw. Gye Shul Park na Ujumbe wake uliofika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 02 Febuari, 2023. Rais wa Kampuni hiyo ameonesha nia ya kujenga Kiwanda cha kuunga Mabehewa hapa nchini, ambayo itaweza kuleta ajira kwa Watanzania, kuongeza Pato la Taifa na pia kuzinufaisha nchi jirani.

 

About the author

mzalendoeditor