Featured Kitaifa

SUALA LA KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO NA WATOTO SIO JUKUMU LA WIZARA YA AFYA PEKEE.

Written by mzalendoeditor

Balozi Batilda Burian Mkuu wa Mkoa wa Tabora akizungumza na wataalam wa Afya kanda ya Magharibi katika ufunguzi wa kikao hicho cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma.

IMG_0058.JPG

Afisa Programu  Wizara ya Afya,Idara ya Afya ya Uzazi ,Mama na Mtoto  Jackline Ndanshau akizungumza na wataalam wa Afya kanda ya Magharibi katika ufunguzi wa kikao hicho cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma

IMG_0076.JPG

Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Dkt.Jesca Lebba akizungumza na wataalam wa Afya kanda ya Magharibi katika ufunguzi wa kikao hicho cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma.

IMG_0183.JPG

Mkunga Mbobezi  kutoka Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga ,Wizara ya Afya Aziza Machenje akichangia mada namna ya kufanya mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi na Watoto wachanga.

IMG_0145.JPG

Mganga Mkuu Mkoa wa Tabora  na Mwenyekiti wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto Kanda ya Magharibi Dkt.Honoratha Rutatinisibwa akichangia mada katika kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi na Watoto wachanga.

IMG_0061.JPG

Katibu tawala Mkoa wa Tabora Dkt.John Mboya akishiriki katika kikao hicho cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma.

IMG_0118.JPG

Afisa Programu ya Saratani ya Uzazi ,Wizara ya Afya,Joachim Masunga akiwasilisha mada katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.

IMG_0120.JPG

IMG_0124.JPG

IMG_0053.JPG

Sehemi ya washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batilda Burian wakati  akizungumza na wataalam wa Afya kanda ya Magharibi katika ufunguzi wa kikao hicho cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma.

IMG_0091.JPG

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batilda Burian akiwa katika picha ya pamoja na  wataalam wa Afya kanda ya Magharibi katika ufunguzi wa kikao hicho cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa mikoa ya Tabora,Katavi,na Kigoma.

…………………………………..

Na.Faustine Gimu,Elimu ya Afya kwa Umma,Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi  Dkt.Batilda  Burian amesema suala la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga sio jukumu la wizara ya Afya pekee hivyo ni muhimu kila sekta kuweka mikakati ya pamoja.

Balozi Burian  amebainisha hayo mkoani Tabora katika ufunguzi wa kikao cha watalaam wa Afya Kanda ya Magharibi inayounda mikoa Tabora ,Katavi na Kigoma cha kujadili mikakati ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga katika kanda hiyo.

“Maelekezo ya Wizara ya Afya ni kuhakikisha kila halmashauri inaweka mikakati ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga hivyo suala hili ni mtambuka sio tu la Wizara ya Afya ni la sekta zote ,sisi viongozi ni kuhakikisha kuwa tunasimamia masuala haya ya Afya ya msingi na afya ya uzazi na watoto ili vifo hivi vipungue ,sababu zinazochangia vifo ni kutokana na kupoteza damu nyingi kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua ,sasa tunafanyaje watu wa kilimo wanafanyaje,katika bustani zao wanakuwa na mbogamboga ,rozela inayosaidia kuongeza damu”amesema.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza vituo vyote vya kutolea huduma katika mkoan wa Tabora vyenye TV  kuweka jumbe zenye maudhui ya Afya ili mwananchi anaposubiri kupatiwa huduma anapata ujumbe sahihi wa Afya  badala ya kusikiliza muziki .

Kuhusu takwimu za vifo vitokanavyo na uzazi katika Kanda ya Magharibi yenye mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi kwa miaka mitatu mfululizo Balozi Dkt.Burian amesema  Mwaka 2019 akina mama wajawazito 210 walipoteza maisha; ambapo, Kigoma vilikuwa vifo 100, Tabora 62 na Katavi 48.

Mwaka 2020 akina mama 235 walipoteza Maisha; ambapo Kigoma vilikuwa vifo 119, Tabora 58 na Katavi 58, na Mwaka 2021 akina mama 174 walipoteza Maisha; ambapo Kigoma vilikuwa vifo 75, Tabora vifo 58 na Katavi vifo 41.

Ametaja sababu kubwa zilizosababisha vifo vya  wajawazito ni pamoja na Kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua,Kifafa cha mimba, Kupasuka mfuko wa Uzazi,Kutokwa na damu nyingi kabla ya kujifungua, Upungufu mkubwa wa damu,Uambukizo wakati na baada ya kujifungua huku hali ya vifo  Mwaka 2020 vitokanavyo na uzazi  kitaifa vilikuwa 1,640 na Mwaka 2021 vilikuwa 1,588.

 

Takwimu za vifo vya watoto wachanga kuanzia siku 0-28 katika Kanda ya Magharibi kwa mwaka 2021  ni watoto wachanga 2,539 walipoteza maisha; ambapo Kigoma vilikuwa ni vifo 1,026, Tabora vifo 954, na Katavi vifo 559  kushindwa kupumua, watoto kuzaliwa  njiti,uambukizi kwa watoto wachanga,na kuzaliwa na uzito pungufu.

Katika kiwango cha mimba za utotoni kanda ya Magharibi Balozi.Dkt.Burian amesema Mkoa wa Katavi ni 25.2%, Tabora 17% na Kigoma 11.9% na hudhurio la kwanza la wajawazito chini ya wiki kumi na mbili kwa mkoa wa Tabora ni 34.4%, Katavi 41% na Kigoma 54.9% na kiwango cha utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango kwa mkoa wa Katavi ni 41%,Kigoma 46.4%,na Tabora ni 60.1%

Hivyo,Mkuu huyo wa Mkoa ametoa maagizo ya Kuongeza uwajibikaji katika usimamizi na utekelezaji wa mipango mikakati itakayoandaliwa ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga, kudhibiti mimba na ndoa za utotoni, elimu ya Afya itolewe kwenye jamii kupitia njia mbalimbali za mikusanyiko ya watu, mashuleni, makanisani na misikitini, vyombo vya habari  na wanaowapa mimba watoto wa shule sheria ichukue mkondo wake ili kudhibiti vitendo  hivyo.

Maagizo mengine ni Mikoa ihakikishe Halmashauri zinakusanya damu ili vituo vya kutolea huduma za Afya hasa Hospitali na Vituo vya Afya viweze kuwa na damu ya kutosha kwa ajili ya kuokoa  maisha ya wajawazito na watoto chini miaka mitano na wagonjwa wengine.

Afisa Programu  Wizara ya Afya,Idara ya Afya ya Uzazi ,Mama na Mtoto  Jackline Ndanshau amesema lengo la kikao hicho kilichoandaliwa na Wizara ya Afya ni kujadili mikakati ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga na kupokea taarifa ya mwaka mzima .

Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Dkt.Jesca Lebba amehimiza umuhimu wa ushirikishwaji katika ngazi mbalimbali za uongozi kujadili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

About the author

mzalendoeditor