Featured Kitaifa

WAZIRI NCHEMBA MGENI RASMI KONGAMANO LA KWANZA LA KODI KITAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

 

KAMISHNA wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,Elijah Mwandumbya, akizungumza  na waandishi wa habari leo Januari 4,2023 jijini Dodoma  kuhusu Kongomano la kwanza la kodi kitaifa litakalofanyika Januari 11, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

……………………………

Na Bolgas Odilo -DODOMA

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu  Nchemba,anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kwanza la kodi kitaifa litakalofanyika Januari 11, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesewa leo Januari 4,2023 jijini Dodoma na Kamishna wa Sera wizara ya Fedha na Mipango,Elijah Mwandumbya wakati akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu Kongomano ambapo amesema kauli mbiu ya kongamano hilo la kitaifa itakuwa ni “Maboresho ya sera kwa maendeleo ya watu”

Mwandumbya,amesema kuwa katika kongamano hilo watajadili hali ya uchumi duniani,fursa na athari zake kwenye sera za uchumi,uwekezaji na biashara nchini Tanzania.

”Kongamano hilo la kitaifa litakuwa la kwanza na litawashirikisha wafanyabishara zaidi ya 300 kutoka kila pande ya nchi na linatarajiwa kufanyika Januari 11 mwaka huu katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.”amesema Mwandumbya

Hata hivyo amefafanua kuwa  kongamano hilo litawakutanisha wataamu wa uchumi, fedha na kodi kutoka serikalini na sekta binafsi ili kujadili mustakabali wa nchi katika kukuza uchumi,biashara, uwekezaji, na kuongeza mapato ya serikali.

”Wadau wanaolengwa katika kongamano hilo ni wale wanaotoka katika sekta binafsi wakijumuisha Wakurungenzi, Mameneja, watalamu wa kodi, wafanyabisahara, makundi maalumu na Mabalozi mbalimbali nchini.”amesema

Aidha amesema kuwa jukumu la Wizara hiyo katika kongamao hilo ni kusikiliza na kukusanya maoni kwa nia ya kuboresha uratibu wa maoni na kuongeza ushirikishwaji wa makundi hayo na utunzi wa sheria.

Amesema maoni hayo yatawasilishwa kwenye kamati ya ushauri wa kodi mapendekezo mbalimbali ya sera za kodi yanayotarajiwa kufanyika katika mwaka wa fedha unaofuata na majukumu hayo yanafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 10(1) cha kanuni za bajeti za mwaka 2015.

About the author

mzalendoeditor